Natafuta kazi ya uhasibu, afisa mikopo au msimamizi wa miradi

mamabaraka

Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
92
Reaction score
14
wana jf, natafta kazi tajwa hapo juu, ninao uzoefu wa usimamizi wa miradi na afisa mikopo kwa miaka miwili, elimu yangu ni advance diploma ya uhasibu, ninao uwezo wa kuongea kiswahili na kiingereza vizuri.Pia binafsi ni mchapakazi mzuri sana, Kwa muajiri anayetafuta watu wa fani yangu tuwasiliane kwa motherofjolly@yahoo.com nimtumie Cv yangu na vyeti. asante sana.
 
Accountant,then una miaka miwil mtaan huna kazi?
 
kipi kinachokushangaza?

Kwanza nina mashaka na elimu unayopata hapo udsm wewe senetor,inaonekana walimu wako wana kaz sana,amekuambia ana uzoefu wa miaka 2 na sio hana kazi kwa mda wa miaka 2,kuwa muelewa! Nina waswas kama ile supp yako umechomoa
 
sa miaka miwil ya uzoefu si ndio tuseme tu hana kazi inayoeleweka,labda alikua anavolunteer au anafanya kama part time?
 
wana jf, natafta kazi tajwa hapo juu, ninao uzoefu wa usimamizi wa miradi na afisa mikopo kwa miaka miwili, elimu yangu ni advance diploma ya uhasibu, ninao uwezo wa kuongea kiswahili na kiingereza vizuri.Pia binafsi ni mchapakazi mzuri sana, Kwa muajiri anayetafuta watu wa fani yangu tuwasiliane kwa motherofjolly@yahoo.com nimtumie Cv yangu na vyeti. asante sana.

Kama ww ni Mkristu wa RC Mkombozi Commercial Bank wametoa kazi unazozihitaji
 
Kwanza nina mashaka na elimu unayopata hapo udsm wewe senetor,inaonekana walimu wako wana kaz sana,amekuambia ana uzoefu wa miaka 2 na sio hana kazi kwa mda wa miaka 2,kuwa muelewa! Nina waswas kama ile supp yako umechomoa
dah huyu senetor bana cjui, ni mtu wa aina gani, mi nlishamwambia anaipenda elimu lakn elimu haimpendi. Vi2 vingne c lazma uchangie unavipotezea tu coz hujui na hutaweza vijua kwa muda huu
 
Kumbe huku udini umetawala? Hii ndio Tanzania tunayoitaka

Mkombozi Commercial Bank ni ya Kanisa Katoliki jimbo la Kuu la DSM, sasa waislam wakafanye nini kny Bank hiyo, Waanzishe yao, ni BENKI YA KANISA
 
wana jf, natafta kazi tajwa hapo juu, ninao uzoefu wa usimamizi wa miradi na afisa mikopo kwa miaka miwili, elimu yangu ni advance diploma ya uhasibu, ninao uwezo wa kuongea kiswahili na kiingereza vizuri.Pia binafsi ni mchapakazi mzuri sana, Kwa muajiri anayetafuta watu wa fani yangu tuwasiliane kwa motherofjolly@yahoo.com nimtumie Cv yangu na vyeti. asante sana.

unataka mahli pa kuiba wewe si bure
 
tatizo la siku hizi wahasibu tumejaa. hivi vyuo ss lazima viangalie background ya mtu yaani kama ulisoma science o level na advance wasikukuchukue katika masomo haya. hivyo wliosoma eca advance ndiyo wangesomea uhasibu. MINADHANI WAHASIBU TUNGEKUWA WACHACHE. lakini kwa hali hii ya ss KAZI IPO
 
mkuu nani alikulazimisha kusoma uhasibu, siyo wewe tu, wengi wanashtuka baada ya kumaliza.
 
Kijana usirudie tena kauli ya kujiita muhasibu(ACCOUNTANT) wewe ni karani wahasibu ni wale wenye CPA! Kwa taarifa yako Tanzania mpaka sasa ina wahasibu 3200 tu!
 
Akili yako itakuwa na matatizo! Mbona unasahau wenye ACCA na sifa zingine kama hizo.Kijana ni mhasibu ambaye hajawa certified na NBAA, CPA zenyewe watu wanapata kwa kubahatisha kama unabisha angalia karibu wote wanaopata CPA wanafaulu kwa daraja la pass yaani C wakati kuna watu wengi walipata GPA nzuri sana vyuoni katika field hiyo.Nadhani wewe utakuwa mmoja wa waliobahatisha.Kwa kukuelimisha zaidi nenda kwenye website ya NBAA ukatafute learning materials for professional exams halafu utajua naongea nini hakika hutaona chochote na kama utapata hakiwezi kukusaidia ukaipata hiyo CPA na hii ndiyo sababu vijana wengi wanafeli mitihani ya Board na hata wanaofaulu ktk professional exams basi wanaishia kupata pass tu yaani C na ndio maana watu wenye mawazo finyu kama yako wanaiona ina thamani sana bila kujali utendaji kazi wa mtu, kwa nyongeza angalia katika field za Udaktari, Uhandisi, Uanasheria, etc mambo yanavyokwenda vizuri.Usimkatishe kijana tamaa kwani ipo siku naye atakuwa certified kwani hata waliopata hiyo CPA walisota sana kwani mfumo mzima wa kupata CPA una complications sana wakati haitakiwi kuwa hivyo.
 
Watu wana madongo kijana endelea kusaka ajila ila kuna projects kama mbili ivi uku kusini kama zikitick ntakustua
Ila check via emplyoment agencies unaweza daka ajira
 
Tukumbukane mkuu, mimi mwenyeji huko, nipo mtwara.
 
Kijana usirudie tena kauli ya kujiita muhasibu(ACCOUNTANT) wewe ni karani wahasibu ni wale wenye CPA! Kwa taarifa yako Tanzania mpaka sasa ina wahasibu 3200 tu!
wewe ni among great thinker aise! Karibu sana Jamvini
 
Back
Top Bottom