Kabla ya kukupatia kazi! Naomba utueleze faida 5 na hasara 5 za kuwafunga mifugo kengere na heleni!
Na maoni yako kwa afya ya mifugo wakivalishwa!
Baada ya kujibu hili kwa ufasaha copy na kupaste PM ukiambatanisha namba yako ya simu na mkoa ulipo
Faida
1.kupunguza wizi na migongano ya mifugo hasa mipakani.
2.kutambua idadi ya mifugo kwa ufasaha na mpangilio sahihi.
3.kupata taalifa za mifugo kwa ufasaha( usahihi)
4.ni utambulisho mzuri na kwa mfugaji hasa kwenye jamii zetu za wafugaji wengi.
5.kumrahisishia mfugaji kutambulika na kukopesheka kirahisi,kwani selikali au taasisi wataelewa kwa urahisi umiliki Halili kupitia Helen
6.itarahisisha kwa selikali kuweka uwiono sahihi wa bajeti pamoja na wataalamu wa mifugo kwa ngazi zote ,,Kijiji ,kata tarafa Hadi ngazi za juu .
Hasara.
1.upotevu wa heleni hivyo kukosa takwimu sahihi.
2.wafugaji wengi ni wakipato Cha chini hivyo kuuza mifugo kiholela na kupotezaa taalifa .
3.kutokuwepo kwa taalifa sahihi za heleni ,,kutoka Kijiji Hadi Kijiji
4.baadhi ya heleni hufutika na kuvunjika hivyo kumbukumbu hupotea
5. Mwizi kutoa na kudai heleni imepotea hivyo kuwekwa nyingine.
Maoni yangu kwa wizara ya mifugo,,watoee elimu kwa wanamchi umuhimu wa heleni
Wahakikishe liwe swala endelevu sio mda mfupi na kutelekezaa
Wawatumie maafisa mifugo waliopo kupata taalifa sahihi kwani mfumo wa wakala unachelewesha na gharama ni kubwa .Asante wakuu.