Hzo Raspberry Pi ni kma vi computer vidogo vyenye uwezo mdogo.
Mara nyingi watu hutumia Raspbian OS (hi ni based on Linux) na mara nyingi vinatumika kwaajili ya kurun bots (automated programs za kufanya kitu flani) au kubeba commands kwaajili ya kuendesha vitu kma robots, na IoT system zingine nyingi.
Sasa sijajua unataka kutumiaje kufanikisha hlo lengo lako.
Kwa huku bongo kuvipata ni shida sana. Wanaokuaga navyo wengi ni wanafunzi wa ICT wanaofanya projects mbali mbali na wao huagiza kutoka nje.
Ungeelezea vizuri zaidi kuwa unataka kutoa elimu bila internet kwa njia gani au software gani?