natafuta kiko

Crucifix

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Posts
1,655
Reaction score
592
Jamani natafuta kiko (mtemba wa kuvutia tumbaku). Babu yangu anasema atanipa laana nisipomletea. Nimejitahidi kumweleza madhara ya tumbaku lakini kasema ameanza kuvuta tangia zama hizo. Kiko chake kimevunjika na hakifai tena anasema alikinunua wakati wa azimio la Arusha. Nimepita madukani hakuna nimeona bure nije hapa, hata kama babu yako alikuachia urithi we niuzie nikamfurahishe babu yangu.
 
Hicho hakifai kuunganisha.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Arusha vipo mkuu jaribu kucheki na watu wa Arusha wakusaidie
 
Duh Mkuu hiyo kitu imenikumbusha mbali sana, Kulikuwa na Mzee jirani yetu, Miaka hiyo ya nyuma, alikuwa akifanya kazi rwele (TRC), alikuwa na Sharubu za haja na kutwa yupo na Kiko yake mdomoni, alikuwa akijiita Mdachi (Mjerumani) .....................
 
nenda kwa mafundi wa kuchoma vyuma, hiyo kazi ni rahisi kwao.
 
Una idea Arusha sehemu gani? Maana kwa kweli nikikipata babu yangu atacheza kiduku siku siku hiyo


Kama ni mwenyeji Arusha nenda kwenye maduka yaliyopo kwenye majengo ya TFA upande wa EXIM bank nakumbuka kuona kiko kikiuzwa hapo. Ni karibu pia na Shoprite
 
Pia unaweza kujaribu pale Mwenge kwa wachonga vinyago kuna siku niliona hiyo kitu.
 
kwa hyo uko serious utalaaniwa kisa kiko au unatuletea mazilizala unataka kutumia mwenyewewe
 
Umetumwa na mganga sio. Waganga wakuua wewe hacha ushirikina
 
Ngoja nikuulizie kwa rafiki yangu mmoja anaitwa Mzee Bantu. Huyu mzee alia ni mkufunzi pale NIT Dar es salaam (amestaafu) na hata tumbaku havuti tena. Sasa sema unazo shilingi ngapi nichome mafuta sasa hivi? Najua atakuwa navyo kadhaa kwenye makumbusho yake.
 
Kinafaa kuvutia bange? Unajaza puli zima humo! Kama inawezekana na mimi nitakitafutaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…