Natafuta Maduka, Vibanda vya Uwakala, Saluni na sehemu ya kuweka Donati zangu

hamza mahundu

Member
Joined
Dec 20, 2018
Posts
58
Reaction score
116
Habari Wakuu,

Natafuta Maduka, Vibanda vya Uwakala, Saluni na sehemu za kuweka Donat zangu.

Donati zangu zauza shilingi 100, nikiweka kwako nitakupa shilingi 20 kwa kila donati.

Nipo Mabibo, Dar es Salaam
 
Hazina skanka ndugu?
Hili naona wengi hawajalielewa. Hakuna mtu atakayekuletea kitafunwa chochote chenye bangi kwa sababu kukitengeza ni gharama kubwa. Vitafunwa vinavyowekwa bangi ni maalum kwa kuuzia watu maalum na bei yake ni kubwa na gharama ya kuvitengeneza ni kubwa. Hakuna mtu mjinga kiasi cha kutumia eg sh milioni 10 atengeneza donut ambazo atauza sh laki moja. Ili iweje sasa? Wewe umeshaona unga wa cacaine ukichanganywa na unga wa sembe madukani ili kuuzia watu? Inawezekana kukawa na bahati mbaya ya mixup lakini inatokea mara chache mno na siyo kwa kudhamiria.
 
nataka vyenye nyama nyama siku ya bday yangu kama vitumbua mia ntalipa kwa 200
 
Weka kwanza picha ya hizo donati tuzione.
Well said
 
tupeane suport wadau sio kuleta maneno ya ovyo kwa kaka mkubwa hapo haipendezi sasa jitu linauliza ina skanka dah ndo mambo gani
 
Mkuu sawa umeeleweka ila ongeza maelezo kidogo kwa mfano kwa siku una uwezo wa kusambaza madonati mangapi na je umelenga watu wa mabibo tu au una uwezo wa kusambaza ndani ya Dar es salaam yote?Hii itakusaidia kuvutia wateja wengi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…