Natafuta mahali ninapoweza kujifunza usindikaji wa maziwa na bidhaa zake

Natafuta mahali ninapoweza kujifunza usindikaji wa maziwa na bidhaa zake

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
7,743
Reaction score
13,657
Salamu!!

Jamani natafuta mahali au chuo au hata mtu binafsi anaweza kunifundisha namna ya kusindika maziwa.

Nimejaribu SIDO wanasema wao wanafundisha usindikaji wa vyakula na milolongo kibao na procedures za kufa mtu.

Kupitia jukwaa hili nisaidieni jamani anayefahamu mahali au mtu binafsi au hata wajasiriamali wanaofundisha au kujihusisha na usindikaji wa maziwa ili kupata bidhaa mbalimbali kama yoghurt, mtindi, samli n.k niunganisheni nao.

Nisaidieni jamani na mimi nataka kwenda uchumi wa kati.

Nawasilisha.
 
balimar,

Jaribu kuulizia SUA, sina uhakika kama wanatoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu hii usidikaji maziwa najua wana ka small processing unit nizamani shawaona wanaprocess na kuuza maziwa in very small scale,,,,unazo option mbili

MOJA....Tafuta kiwanda chakusindika maziwa, uombe kujitolea kwa muda utapata hiyo elimu, kuna small scale producers ukienda kilimanjaro machame kipo kikundi cha akinamama...kwa Dar es salaam mtafute MKE wa msaafu wa TAnzania Airport Authority... NDUGU TESHA WANAYOBIASHARA YA KUISNDIKA MAZIWA
PILI...Nenda SUA tafuta mtaalamu mwenye huo ujuzi ongea naye akuandalie tailor made course kwajili ya kusindika maziwa

Ukishindwa zote::::::chukua kalamu na daftari,, nenda chuo kikuu YOU TUBE....utapata kila kitu,,,

Ukishafanikiw aujehapa kushukuru
Tembelea

Sido ndio aliepewa jukumu la kutoa mafunzo kwa wazalishaji wadogo na Wa kati.
Wana taratibu zao ingawa taratibu zao ni kukusanya wahitaji kwa pamoja kisha wakapewa gharama za mafunzo wakishakulipia kama kikundi ndipo tarehe ya mafunzo hutolewa.
Namna nyingine ikiwa unauhitaji individually na wakati huo sido hawajawa na uwezekano Wa kupata wanafunzi wengi basi ofisi ya sido hukuungisha na mkufunzi kisha ufanye nae makubaliano ya gharama individually kisha atakupatia mafunzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
balimar,

Soma hiyo makala na umtafute jamaa kaweka namba zake

Avriel,
Mkuu SIDO kwani huwa wanakwama wapi?
Nashangaa kozi nyingi ukiulizia hupati majibu ya kueleweka. Inasikitisha vitengo vingi havifanyi kazi. Mfano, utengenezaji wa bidhaa za ngozi, Batiki, mishumaa, chaki, kozi nyingine mpaka ungoje miezi 6, ukirudi unaambiwa bado wanafunzi hamna.
 
Sido wanaweza tangaza mafunzo na wahitaji wakakosekana, sasa hapo aliekwama ni sido au mwananchi?
Wakati individual anatafuta mafunzo sido inaorganise wanafunzi wawe wengi ili kubalance gharama za mafunzo.
Pia sido wanakupa options za kutafuta wakufunzi binafsi wao watafacilitate taratibu muhimu......ivo yaani.

Mkuu, ukiangalia taasisi nyingine hazina tatizo la kuwa na wanafunzi. Kwa mfano vyuo vya ufundi binafsi. SIDO bei zao ni nzuri na mafunzo ni muda mfupi lakini wanaokwama ni wao na sio wananchi. Vitu wanavyofundisha havifanyiki pale. Vinafanyika maonyesho yanapokaribia ili wajipatie ushindi. Kwa mfano nilitegemea kama ni usindikaji, wawepo wasindikaji pale, kama ni bidhaa za ngozi wawepo watengenezaji pale, kama ni batiki, tufike pale wawepo wanao tengeneza. Hivi vitu havifanyiki pale. Nafikiri wangeweza kupromote waliowapa mafunzo wavifanye pale, at least awe na center ya wajasiriamali pale.
 
balimar,

Mkuu kama uko dar es salaam ukivuka lile daraja la nssf kama unaenda kigamboni kuna mahali pana bendera za chama cha mapinduzi na mashina ya jumuiya ya wazazi. Ingia hapo hiyo njia nenda utakuta msikiti na soko. Opposite na huo msikiti pana mjasiriamali ana kiwanda kidogo cha maziwa. Yuko vizuri sana mkuu. Anatengeneza flavoured milk. Hapo utajifunza mengi sana
 
balimar,

Hicho kiwanda chake kinaitwa Tamu Milk. Unaweza ukacheki kwenye social media ukawasiliana nae
 
Mkuu, ukiangalia taasisi nyingine hazina tatizo la kuwa na wanafunzi. Kwa mfano vyuo vya ufundi binafsi. SIDO bei zao ni nzuri na mafunzo ni muda mfupi lakini wanaokwama ni wao na sio wananchi. Vitu wanavyofundisha havifanyiki pale. Vinafanyika maonyesho yanapokaribia ili wajipatie ushindi. Kwa mfano nilitegemea kama ni usindikaji, wawepo wasindikaji pale, kama ni bidhaa za ngozi wawepo watengenezaji pale, kama ni batiki, tufike pale wawepo wanao tengeneza. Hivi vitu havifanyiki pale. Nafikiri wangeweza kupromote waliowapa mafunzo wavifanye pale, at least awe na center ya wajasiriamali pale.
Kuna baadhi ya mikoa wanazo hizo workshops na incubation rooms za watu kujifunzia kwa vitendo.
Otherwise wanahitaji maboresho zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom