Mkuu SIDO kwani huwa wanakwama wapi?
Nashangaa kozi nyingi ukiulizia hupati majibu ya kueleweka. Inasikitisha vitengo vingi havifanyi kazi. Mfano, utengenezaji wa bidhaa za ngozi, Batiki, mishumaa, chaki, kozi nyingine mpaka ungoje miezi 6, ukirudi unaambiwa bado wanafunzi hamna.
Sido wanaweza tangaza mafunzo na wahitaji wakakosekana, sasa hapo aliekwama ni sido au mwananchi?
Wakati individual anatafuta mafunzo sido inaorganise wanafunzi wawe wengi ili kubalance gharama za mafunzo.
Pia sido wanakupa options za kutafuta wakufunzi binafsi wao watafacilitate taratibu muhimu......ivo yaani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna baadhi ya mikoa wanazo hizo workshops na incubation rooms za watu kujifunzia kwa vitendo.Mkuu, ukiangalia taasisi nyingine hazina tatizo la kuwa na wanafunzi. Kwa mfano vyuo vya ufundi binafsi. SIDO bei zao ni nzuri na mafunzo ni muda mfupi lakini wanaokwama ni wao na sio wananchi. Vitu wanavyofundisha havifanyiki pale. Vinafanyika maonyesho yanapokaribia ili wajipatie ushindi. Kwa mfano nilitegemea kama ni usindikaji, wawepo wasindikaji pale, kama ni bidhaa za ngozi wawepo watengenezaji pale, kama ni batiki, tufike pale wawepo wanao tengeneza. Hivi vitu havifanyiki pale. Nafikiri wangeweza kupromote waliowapa mafunzo wavifanye pale, at least awe na center ya wajasiriamali pale.