Kuna wakati Yesu alikutwa akiwa na watu huenda wanafanana na hao marafiki zako.Watu wakashangaa kwanini anaambatana na watu kama hao.Aliwajibu: mtu mzima hahitaji daktari bali mgonjwa na nilkuja kuwakomboa wenye dhambi.Hivyo utagundua kuwa watu kama rafiki zako huwa hatujitengi nao ila tunajichanganya nao.Nenda nao popote wapende.mkifika sehemusehemu wao wakiagiza bia wewe agiza soda,watashangaa,utawaeleza sababu ya kubadilika iwapo watakuuliza.wakifanya uzinzi wewe usifanye. Oda ya KUKU choma au supu au nyama choma ikifika mezani wao watakapovamia na kuanza kula,wewe fumba macho SALI kabla ya kula. Hapo utakuwa umefanya kazi kubwa zaidi ya mahubiri, utakuwa TAA na chumvi kwao, itafika wakati watagundua kuwa maisha yako ni bora kuliko wao.HATUWACHUKII AU KUWATENGA WENYE DHAMBI.BALI TUNAICHUKIA NA KUITENGA DHAMBI.Yesu angetutenga au kutuchukia ANGEKUJA duniani?...........HATA HIVYO HUO NI MTAZAMO WANGU.JICHANGANYE NAO TU NA USIACHE MAOMBI.