Natafuta mawakala wa hii kampuni..

kiogwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
3,757
Reaction score
4,940
Wakuu hili jukwaa limekua jukwaa la kusaidiana mambo mengi sana. Msimu huu wa kilimo nimeandaa shamba kubwa la ufuta.shida yangu kubwa natafuta mwakala wanaosambaza hii dawa inaitwa (ROUNDUP) hii dawa nasikia ni nzuri kwa kuua magugu shambani au km kuna dawa inayoizidi hii naomba msaada wenu wa utaalamu nahitaji nyingi sana
 
Wataalam wa madawa ya kilimo na kilimo kwa ujumla naombeni msaada wenu nipo ktk maandalizi ya kilimo hii dawa nimeambiwa ni nzuri sana inatengenezwa Nairobi mwenye kujua ofisi au anuani ya wakala anayezosambaza hii sumu ya magugu
 
Mkuu kiogwe nakushauri uwende agrovet yeyote iliyo karibu na wewe watakupa hints za hao giant suppliers wa roundup na hata kuhusu mbadala wa hiyo roundup.
Kwa ninavyo jua mimi itaku cost sana kuua magugu kwa roundup make inabidi upige mara mbili kama lengo lako ni kuua kabisa magugu yote.
Firstly utalima na kusubiri magugu yaote ndo upige dawa then magugu hayo yakifa unasubiri mengine yatakayo ota uyaache mpaka yatoe mbelewele ndo una spray tena hiyo roundup. Hapo utakuwa umeua kizazi chote cha magugu ndani ya shamba lako.
Nahisi kutakuwa na side effect kwa rutuba ya asili ndani ya shamba! (But i stand to be corrected on this).
Kila la kheri mkuu ktk ukulima wako!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu KISIMA nashukuru sana kwa ushauri wako lakini hiyo sehemu ninayolima ndio kilimo chao cha kutumia kuua majani ndio unapanda.nalima ufuta nimezunguka sana hapa Dar nimeyaona madawa ya kuua majani ni mengi sana sasa na mimi ni km nimekalilishwa na wenyeji wa huko wao wanaamini roundup ndio dawa nzuri.naomba km kuna dawa yoyote nzuri na kari zaidi ya hiyo naomba wadau mnisaidie wakara na aina ya dawa.KISIMA naomba usinichoke Mkuu km una wataaram wa hayo madawa niulizie ipi ni kari sana itakayonisaidia nalimia Liwale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…