Natafuta mawakala wa movie za kutafsiri

Natafuta mawakala wa movie za kutafsiri

LOYAL AMANI

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
1
Reaction score
10
Habari za leo wanajamii.

Kati ya post zangu za hapo nyuma niliongelea application niliyotengeneza ya kuondoa sauti za waigizaji kwenye movie za netflix ili niweze kuweka sauti za kiswahili.

Kwa ufupi natafsiri movie kama wanavyofanya kwenye tv ila niuze mtaani. Tayari nimemaliza kufanya debugging ya program yangu na nina sample kadhaa za trailer nilizozitoa sauti, ili niweze kuingia studio kurekodi sauti za kiswahili.

Kwa sasa ninatafuta mawakala wa kuuza hizi movie kila wilaya; nimeona nifanye hivi ili iwe rahisi movie hizi kupatikana kuliko kuuza kariakoo ambapo wateja wa mikoani wangechelewa kuzipata au wangepata inferior quality kwa wanaotoa copy kariakoo.

Nataka niwe na wakala mmoja kwa kila wilaya ambaye nitamuuzia master kwa bei ndogo tu kisha yeye atawauzia wenye library za movie ndani ya wilaya yake. Mtu yeyote atakaye nitafuta kuulizia movie ataelekezwa kwa wakala aliyeko wilayani mwake. Wakala atakuwa na uhuru wa kupanga bei anayouza cd kwa wenye library kulingana na gharama zake za biashra.

Ni vyema wakala awe anamiliki library tayari ili awe mzoefu katika biashara. Kwenye post hii nime-attach trailer ambayo nimeitoa sauti ila bado sijaiweka sauti za kiswahili kwa wale watakao penda kujihakikishia kuwa ninachokisema ni kweli.

Kama unamiliki movie library au unamfahamu mtu anayemiliki library tafadhali mfikishie ujumbe huu maana naamini ni fursa nzuri kwa vijana wanaotafuta kujiajiri.

Kwa wale ambao wangependa kuchangamkia fursa hii tafadhali nitumie message whatsapp kwa simu namba +255624154919 ukieleza upo wilaya gani na kwamba ungependa kuwa wakala wa movie za Dj Titto. Kama una rafikiau jamaa mwenye library tafadhali mtumie au mwonyeshe clip ya trailer niliyoiweka kwenye hii post; kama akipenda kuona trailer nyingine pia niulizie.

Natanguliza shukrani.

NB: Ninaomba wanajamii mnisaidie kuisambaza hii video. Nnitapost video nyingine siku zijazo hasahasa studio wakishamaliza kuingiza sauti za kiswahili ili mpate picha halisi ya kazi tunayojaribu kuifanya.
 
Attachments

  • Jamii forums ad 3.mp4
    64.4 MB
Shida inapokuja ni pale mkiingiza sauti zenu na ubora wa muvi unakuwa mbovu.
Yaani muvi inakuwa na ukungu alafu mnatafsiri matendo ya muvi na sio wanachojadili waigizaji wa muvi.
MPAKA MNAPOTEZA UHALISIA WA MUVI.

WENDA👉👉 WEWE UTAKUWA TOFAUTI.
 
Habari za leo wanajamii.

Kati ya post zangu za hapo nyuma niliongelea application niliyotengeneza ya kuondoa sauti za waigizaji kwenye movie za netflix ili niweze kuweka sauti za kiswahili.

Kwa ufupi natafsiri movie kama wanavyofanya kwenye tv ila niuze mtaani. Tayari nimemaliza kufanya debugging ya program yangu na nina sample kadhaa za trailer nilizozitoa sauti, ili niweze kuingia studio kurekodi sauti za kiswahili.

Kwa sasa ninatafuta mawakala wa kuuza hizi movie kila wilaya; nimeona nifanye hivi ili iwe rahisi movie hizi kupatikana kuliko kuuza kariakoo ambapo wateja wa mikoani wangechelewa kuzipata au wangepata inferior quality kwa wanaotoa copy kariakoo.

Nataka niwe na wakala mmoja kwa kila wilaya ambaye nitamuuzia master kwa bei ndogo tu kisha yeye atawauzia wenye library za movie ndani ya wilaya yake. Mtu yeyote atakaye nitafuta kuulizia movie ataelekezwa kwa wakala aliyeko wilayani mwake. Wakala atakuwa na uhuru wa kupanga bei anayouza cd kwa wenye library kulingana na gharama zake za biashra.

Ni vyema wakala awe anamiliki library tayari ili awe mzoefu katika biashara. Kwenye post hii nime-attach trailer ambayo nimeitoa sauti ila bado sijaiweka sauti za kiswahili kwa wale watakao penda kujihakikishia kuwa ninachokisema ni kweli.

Kama unamiliki movie library au unamfahamu mtu anayemiliki library tafadhali mfikishie ujumbe huu maana naamini ni fursa nzuri kwa vijana wanaotafuta kujiajiri.

Kwa wale ambao wangependa kuchangamkia fursa hii tafadhali nitumie message whatsapp kwa simu namba +255624154919 ukieleza upo wilaya gani na kwamba ungependa kuwa wakala wa movie za Dj Titto. Kama una rafikiau jamaa mwenye library tafadhali mtumie au mwonyeshe clip ya trailer niliyoiweka kwenye hii post; kama akipenda kuona trailer nyingine pia niulizie.

Natanguliza shukrani.

NB: Ninaomba wanajamii mnisaidie kuisambaza hii video. Nnitapost video nyingine siku zijazo hasahasa studio wakishamaliza kuingiza sauti za kiswahili ili mpate picha halisi ya kazi tunayojaribu kuifanya.
Vip hii project ipo au ilikufaa?!
 
Back
Top Bottom