Natafuta mbia/ business partner

Natafuta mbia/ business partner

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Wakuu nina eneo la robo tatu eka Morogoro maeneo ya Nanenane karibu na shule ya sekondary Tubuyu. Ni eneo lililopimwa na documents zake ninazo. Kwa sasa nimelizungushia ukuta lote na kuweka geti kabisa nikaishiwa fedha - so it's well secured! Ni eneo zuri linalofaa kwa biashara ya:
1.Hostel
2.Apartments
3.English medium school, chuo/training centre mfano computer/secretarial services n.k
4.Guest house
5.Bar
6.Ukumbi
NB: Hivi vitatu vya mwisho eneo linatosha kukaa vyote kwa pamoja

Kwa kuwa kwa sasa sina uwezo wa kifedha, naplan kuweka kuku (broilers, layers na wakienyeji) - maoni ya wadau hapa JF yameni-impress sana!

Ila natafuta mtu/taasisi tuweze kuingia ubia tuwaangalie uwezekano wa kufanya hizo biashara nilizotaja 1-6 hapo juu.
Tutawekeana mikataba ya kisheria ili kila upande uwe na peace of mind.

Karibu tuunganishe nguvu! Aliye serious tuwasiliane kwa PM
 
Wakuu mbona mnasoma tu na kukimbia??? jamani nipeni hata mawazo basi namna ya kufanya ili eneo langu liwe profitable!
 
Sio kwamba wanakimbia uwezo mdogo. Hayo mambo yanahitaji kujipanga vya kutosha.

Mkuu kana unayo title deed ya eneo kwa nini uweke msingi wa kimojawapo unachotaka kufanya then nenda bank kakope.

Nanenane ni one of prime areas in Morogoro. Hivyo huna haja ya mmbia. karibu tukutengenezee bankable business plan.
 
Nashukuru umenipa wazo mkuu Kichakoro. Honestly title deed sina, kwa sasa nina ofa tu, ila naweza kuanza mchakato wake. Ila hata nikipata hiyo title deed si nasikia bank wanataka uwe na biashara tayari?
 
mpaka apo umepiga hatua kubwa sana. usitafute mbia. tafuta title deed then kutana na real estate advisers, financial advisers na legal advisers wakupe ushauri wao wa kitaalamu. Mana kuna watu mate yanawatoka wakisia ardhi iliyo hot kama iyo.
 
Duh! mkuu rolla hebu nipe hints zaidi, nahisi una mwanga zaidi ktk hii area
 
Back
Top Bottom