wana jamii nimeona tangazo la mbwa nikakumbuka kuwa nilikuwa natafuta Mbwa kwa mda mrefu sana kwa ajili ya ulinzi wa nyumba wakati nipo kazini BILA MAFANIKIO.
NAPENDELEA ZAIDI AINA YA German Shepherds ILA KAMA KUNA AINA NYINGINE SIO MBAYA
KAMA KUNA MTU ANAMAELEZO WAPI WANAPATIKANA AU WANAUZWA KWA BEI NZURI NITAFURAHI NAHITAJI 2 WASIWE WAKUBWA WAWE WADOGO CHINI YA MIEZI 4
Mkuu kuna bwana mmoja ana shamba la mbwa wazuri sana German Shepherds yuko kimara mwisho, Dar es salaam, anauza laki tatu na nusu hadi nne inategemea, ni wazuri kwa kweli nilinunua kamoja hakajanisumbua hadi leo, if interested nikutumie namba yake
Wakuu hata mimi nawahitaji hao mbwa ile mbaya yake!Mkuu SOKWE WA MJINI naomba namba ya huyu mtu mwenye hao walinzi please!ntakushukuru sana kwa msaada wako
Aje nimpe wale na yeye gari yake(maeneo ya plastic) kama walivyokula yangu, wakipata njaa wanakula hadi nyumba ila ni walinzi wazuri kusema kweli na wanafundishika.