Natafuta mchumba wa kuja kuwa mke wangu

Natafuta mchumba wa kuja kuwa mke wangu

Product

Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
68
Reaction score
66
Mimi ni kijana wa takribani miaka 29 sasa,lengo la kuanzisha uzi huu wala si kitu kingine zaidi ya kutafuta mwenza ambae baadae atakuja kuwa Mke wangu

Najua kwa sasa atapopatikana kwasababu hatujajuana nitapenda tufahamiane kwanza,kwa kushirikiana katika biashara ndogo ndogo ninazofanya mimi

Kupitia biashara nitamfahmu anapenda nini na yeye atanifahamu napenda nini

SWALI : Atafanya biashara kama mfanyakazi au mpenzi?

JIBU : kwa mwanzo huu atakua na mimi kama patner tu kibiashara so kitakachopatikana jioni tutagawana 50/50

Tutakaporidhika na ushirikiano wetu katika maisha/biashara kwa ujumla ndio tutakua wapenzi RASMI.

SIFA:

Kabila : lolote

rangi : yeyote

Awe mpole
Asiwe maneno mengi
Ajue kuongea ninapokosea/sio nikosee yeye aniangalie tu HAPANA
Asiwe bonge/kibonge
Awe na umbo la kidada na sio kimama
Awe anasuka hata kama hasuki napenda asuke
Asiwe mpenda makucha wala makope bandia
Asiwe mrefu toluuuuuu..awe wastani kama wadada wengi wa sasa walivyo (sio mfupi wala mrefu)

DINI: MKRISTO

sifa zangu

dini: mkristo
Rangi: white maji yakunde (sijui hata nipoje poje)
Elimu: Form 4
Urfu: size wastani
Sio mnene ni mwembamba flani hivi
Mfanyabiashara

Sifa zingine tutaelezana kwa picha baada ya kukutana whatsapp huko,kwa yeyote alie serious naomba asisite kuja PM

NAPENDA mwanamke mchapakazi na asie chagua kazi...

Niko serious kuliko maelezo...

Asije pm mtu ambae hayupo serious au wa majaribio.

Asanteni kina dada.

WENU

KAKA MTAFUTA MWENZA
 
Mimi ni kijana wa takribani miaka 29 sasa,lengo la kuanzisha uzi huu wala si kitu kingine zaidi ya kutafuta mwenza ambae baadae atakuja kuwa Mke wangu
Hahahaha!!! Mkuu, vijana mmeharibika sana. Ina maana kuna wengine wanatafuta wachumba wa kutokuja kuwa wake? Hatari
 
'Sijui hata nipoje nipoje' Ina maana hiyo rangi umenipata siku si nyingi au?

'Sifa zingine tutaelezana kwenye picha whatsapp' Ngastuka. Isije kuwa mnataka kuonyeshana sehemu za siri nyie?
 
Hahahaha!!! Mkuu, vijana mmeharibika sana. Ina maana kuna wengine wanatafuta wachumba wa kutokuja kuwa wake? Hatari
ndio mkuu,wapo wengine kwa ajili ya sex mkimaliza kila mtu na njia yake
 
'Sijui hata nipoje nipoje' Ina maana hiyo rangi umenipata siku si nyingi au?

'Sifa zingine tutaelezana kwenye picha whatsapp' Ngastuka. Isije kuwa mnataka kuonyeshana sehemu za siri nyie?
Hapana mkuu..bado hatujawa wapenzi picha za utupu siwezi hitaji na hata yeye akihitaji sitomtumia
 
ndio mkuu,wapo wengine kwa ajili ya sex mkimaliza kila mtu na njia yake
Sasa huyo mchumba au changudoa? Ukisha sema unatafuta mchumba basi tunajua wa kuoa Mkuu, Ila nakushauri mchumba hatafutwi, anakuja katika mazingira usiyotarajia na anaweza kuwa mtu usie wazia hata kuoa lakini unamfahamu tayari/. Ukitafuta mara nyingi utaoa asiyestahili. Nakushauri usitafute, acha itokee ukakutana naye bila hata kutarajia
 
Nenda kanisani kila wiki japo miezi mitatu usikosekane,Ukikosa waimba kwaya basi hata waumini wa kawaida nao utawapata tu
 
Sasa huyo mchumba au changudoa? Ukisha sema unatafuta mchumba basi tunajua wa kuoa Mkuu, Ila nakushauri mchumba hatafutwi, anakuja katika mazingira usiyotarajia na anaweza kuwa mtu usie wazia hata kuoa lakini unamfahamu tayari/. Ukitafuta mara nyingi utaoa asiyestahili. Nakushauri usitafute, acha itokee ukakutana naye bila hata kutarajia
hivi ni kweli mkuuu?
 
Unafanya biashara ndogo ndogo zipi wewe mfanyabiashara? Hebu weka wazi hapa kabla hatujawaruhusu hao dada zetu kukufuata huko pm!
 
hivi ni kweli mkuuu?
Amini nakuambia.Oa mtu unaempenda sio mwenye sifa ulizoorodhesha. Ukikutana na unaempenda hizo zifa wala hutazikumbuka. Na anaweza kuwa mweusi Msudan cheupe dawa! Usioe sifa, oa rafiki ambae mnapendana.
 
hahahah siku biashara zimebuma ndoa chalii..khaa wadada kuweni makini..hii ni kujivika suicide bomb..lol
 
Amini nakuambia.Oa mtu unaempenda sio mwenye sifa ulizoorodhesha. Ukikutana na unaempenda hizo zifa wala hutazikumbuka. Na anaweza kuwa mweusi Msudan cheupe dawa! Usioe sifa, oa rafiki ambae mnapendana.
Mkuuu kwa comment hiii nashawishika kukiri kwa binafsi yangu bila kulazimishwa na mtu yeyote kwamba SIHITAJI TENA MTU AJE PM nimeuelewa ushauri wa ndugu yangu hapa nimeutafakari kw kina nimeridhika kwa aliyonishauri.

ASIJE MTU YEYOTE PM asante mkuu Synthesizer umenifundisha kitu leo.
 
Amini nakuambia.Oa mtu unaempenda sio mwenye sifa ulizoorodhesha. Ukikutana na unaempenda hizo zifa wala hutazikumbuka. Na anaweza kuwa mweusi Msudan cheupe dawa! Usioe sifa, oa rafiki ambae mnapendana.
very true
 
Back
Top Bottom