Natafuta 'Mentor' mzoefu wa kuuza na kununua viazi mviringo na kuvisafirisha

shankima

Member
Joined
Aug 3, 2017
Posts
8
Reaction score
3
Jamani,

Mimi ni kijana wa kitanzania nahitaji kujikwamua kiuchumi na nimepata wazo la kwenda kuchukua viazi mviringo Mbeya na Iringa na kuja kuviuza mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

Shida yangu kubwa nahitaji nimpate 'Mentor' au mtu aliyewahi kufanya hiyo biashara angalau anipe moja mbili tatu kuhusu hii biashara hususani changamoto zake, sehemu mzigo mnapochukulia, gharama zake, hata na faida zake.

Nitashukuru sana wakuu endapo nitapata msaada kwa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Peleka mtwara hutajuta.

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 
Reactions: amu
Nenda mabibo sokoni unaongea na Dalali mzoefu! Kikubwa hapo wewe unapaswa kujua
Gunia la viazi bei gani shambani,
Sokoni bei gani,
Fuso inajaza gunia ngapi,
Usafiri sh ngapi,
Ushuru wa ahambani & sokoni,
Gharama ndogo ndogo kama magunia, kamba, kupakia & kupanga, kushusha na Posho ya Dalali sh ngapi!
Those are basic...mi naleta bidhaa nyingine kwa viazi sina details za kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh. Hakuna kosa kubwa atakalofanya kama kuulizia kwa dalali. Madalali ni walaghai sana na akijua mtu ni mgeni kwenye biashara atampiga sana. Haya mambo unaweza kuyafanya kimya kimya tu.

Unaenda sokoni unafanya utafiti wako, unatenga nauli unasafiri viazi vinapotoka unafanya utafiti kabla ya kuanza biashara.
 
Nakubali hii mzee. Otherwise huyo dalali mjuane personally ndio akupe ABC za ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama upo fresh Shamba nakupeleka boss

Sent from my Infinix HOT 4 using Tapatalk
 
Mkuu weka hayo mazao mengine tufaidike
 
Hii biashara hata mi nakukubali Sana, tufungueni wazee
 
Nione Pm mawasiliano ya mtu ninae mfahamu, ambae anaweza kukusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…