Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha Ardhi Dar es Salaam.Ninachukua Bachelor of Science in Accounting and Finance(BAF).Sijafanikiwa kupata mkopo japo nimejitahidi kufatilia.Kwasasa ninasomeshwa na wajomba zangu ambao nao wana majukumu mengi kw kipindi hiki hivyo kufanya msaada wao kupungua.Wananisomesha wao kwasababu mama yangu alifariki tangu nipo darasa la kwanza na baba yangu hana msaada tena kwangu na dada yangu toka kipindi hicho na yeye alishaoa mke mwingine.Kuhusu ufaulu wangu ni mzuri,O-level nilipata division 1,Advance level nilipata division 2 na hata chuo kwa mwaka wa kwanza nimekuwa best student kwenye department judged by overall performance.Natokea wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.