Natafuta miti ya matunda yafuatayo:

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
156
Ndugu wana JF, natumai hamjambo!
Naomba mnisaidie wapi naweza kupata miti ya matunda yafuatayo? Nahitaji angalau miti miwili katika kila aina.
Nahitaji mnisaidie kunielekeza nitakapozipata, contacts na if possible na bei zake:

(1)Zabibu (nyeusi na za kijani) - jumla miti minne
(2)Strawberry - miti miwili
(3)Zeituni - miti miwili
(4)Dates (tende) - miti miwili
(5)Apples (tufaa) - miti miwili
(6)Pears - miti miwili
(7)Pomegranate (komamanga) - miti miwili
(8)Mulberry (forosadi) - miti miwili
(9)Tangarine (chenza) - miti miwili
(10)Na miti ya matunda mengine mengi kadiri mtakavyoona yatanifaa, sana sana mimea inayostawi sehemu ya joto - nataka niipande Mtwara.

Nitashukuru.
 
Ngoja nami niisubiri maana mingine sijawahi hata kuiona maishani kama 'zeitoon'.
 
Straberry (mafurusadi) -

Miche mingi ya Matunda ipo sana Arusha na Lushoto sijui kwa hapa Dar.

Ngoja tusubiri
 
kama uko dar,nenda bonde la kawe kama unaelekea Tegeta(karibu na tangi bovu) yapo aina mbali mbali bei ni maelewano
 
kama upo dar nenda kurasini pale wapo radio utapata msaada zaidi
 
apple na pears kwa mTwara haitafaa. inahitaji sehemu za baridii. au kama unaitaka iwe kama mapambo tu!
 

Che Guevara: Kuna miti uliyotaja ambayo sidhani kama itaweza kuzaa matunda katika hali ya joto kama hili, mfano strawberries. Jaribu kutembelea nursery ya SUA (horticulture) hapo zamani walikuwa wanauza miche aina tofauti tofauti.

Au, tafuta mtaalamu wa mambo ya nursery au mwenye nursery akuatikie miche unayotaka halafu utamlipa, kwani kuatika miche ya miti ina utaalamu wake.
 
Nawashukuru ninyi nyote mliochangia katika mada hii.
Nitafuata ushauri wenu!
Ngoja nijaribu tu na miti mingine hata kama ikitoa matunda mawili kwa mwaka poa tu (itakuwa sehemu ya mapambo pia).


''The revolution is not an apple that falls when it is ripe. You have to make it fall''
 
kwa kweli katika miti uliyouliza sijawahi sikia kama kuna miti ya zeituni hapa kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…