Natafuta mke (25yrs - 30yrs)

Mwagito84

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
235
Reaction score
709
Nina miaka 35 mkristu wa madhehebu ya RC. Nina mtoto mmoja wa kike 7 aged na naishi IRINGA. Natafuta mke mwenye sifa zifuatazo
. Awe mkristo wa dhehebu lolote ila kama ni islamic asiadhiri maisha yangu kwa imani yake
. Awe na akili, mbunifu na mtu anayependa kufanya kazi na kujituma kwenye majukumu yake bila kisimamiwa
. Awe mtulivu na asiwe muongeaji sana
. Ajue maana halisi ya maisha/ndoa na familia
. Awe na adabu, msikivu na mwenye staha. Asiwe na gubu
. Rangi yoyote ila asiwe mwembamba sana. Akiwa na umbo la kiafrika itakuwa safi zaidi.
. Asiwe na mtoto zaidi ya mmoja
.Ajue kupika na awe mama kwelikweli

Incase tuwasiliane. DM
 
Picha
 
Kila la heri juu jirani yangu, nakupongeza umekuja na ID yako ya siku zote
 
kuna binti alikua anatafuta mme wa miaka 33-38 naomba kama upo karibu naye mshtue... mume kajileta huku. [emoji23][emoji23]
 
Umri wote huo ulikuwa hujaoa tu?

"Nyie ndio mmeharibu dada zetu&mama zetu wadogo arafu saizi mnaanza kusumbua wana jamvi huku!"
 
Yaani wanawake walivyojaa km Mchanga wa bahari, Wafupi a. k. a mbilikimo, warefu wembamba, warefu vibonge, Wale wa saizi ya kati, Wale vipotabo ambao Unaweza kuwaficha hata kwenye mfuko wa suruali, incase kuna Shida ya usalama, Weusi km lami, weupe, Maji ya kunde, Wenye pua za kuchongoka, wenye pua kubwa km yangu, Wale wenye midomo mipana, midomo myembamba, Macho makubwa ya kulegea, macho madogo saizi ya Funza wote Wanapatikana, inakuwaje Unakuja kujianika hapa Mnyalukolo???.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…