Miaka 27 unatafuta mke mtandaoni ???
Kwamba unaishi porini ?
Kwamba hujawahi kushiriki tendo na mwanamke/wanawake ? (Oa mmoja ya wale uliolala nao).
Nashangaa sana nikiona kijana wa miaka 25+ anatafuta mwanamke wa Kuoa mtandaoni au anamuagiza mtu "nitafutie mke wa kuoa huko" au wengine utakuta anapeleka posa kwa mwanamke ambaye hajawahi kuongea naye ila kwakua anaona anapendeza mzuri yeye anapeleka proposal tu.
N.B, vilio kwenye ndoa havitoisha msipoacha huu ujinga wa kutafuta mke/wake mitandaoni na kuoa msiowafahamu.