Natafuta mkopo wa kilimo au ufugaji wana jamvi

ydalnorI

Member
Joined
Mar 21, 2019
Posts
37
Reaction score
26
Salam kwenu wakuu.

Mimi ni mfugaji/mkulima ambaye nimepitia changamoto nikakwama kimtaji. Naomba kama kuna mdau humu ambae anaweza kunisaidia jinsi ya kupata mkopo au udhamini ili nibust ufugaji wangu na kilimo pia. Nina heka 50 za shamba ambalo nahitaji kupanda maharage msimu ujao na kuku wangu wa layers walikumbwa na balaa ambalo sikuweza kuokoa chochote. Ujuzi na uzoefu ninao ninakosa tu mtaji wana jamvi wenzangu.

Naishi Arusha kama kuna yoyote ambae anaweza kunisaidia kwa hali na mali nita shukuru na kumuombea mema mengi yamuelekee.
Asante
 
Umri wako?
Uzoefu katika shughuli za kilimo?
Securities?

Waone bank ya kilimo. Usisite nenda kama unania ya dhati
 
Kama unauzoefu na hiyo kazi na una mashamba usisite kwenda bank ya wakulima siku hizi hawana magumashi na uhakika watakusaidia
 
Asante sana mwana jamvi , bank ya kilimo hii ipo kila mkoa kweli au ni Dar tu? Mimi niko Arusha , naomba usinichoke nielekeze how to go tafadhali
 
Salam kwenu wakuu.
Mimi ni mfugaji/mkulima ambaye nimepitia changamoto nikakwama kimtaji. Naomba kama kuna mdau humu ambae anaweza kunisaidia jinsi ya kupata mkopo au udhamini ili nibust ufugaji wangu na kilimo pia. Nina heka 50 za shamba ambalo nahitaji kupanda maharage msimu ujao na kuku wangu wa layers walikumbwa na balaa ambalo sikuweza kuokoa chochote. Ujuzi na uzoefu ninao ninakosa tu mtaji wana jamvi wenzangu.
Naishi Arusha kama kuna yoyote ambae anaweza kunisaidia kwa hali na mali nita shukuru na kumuombea mema mengi yamuelekee.
Asante
Onana na Bashe haraka sana.
 
Ngoja waje kukupa muongozo... Ila kama una nia kweli, nenda kwenye taaisi zinazokopesha...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom