Natafuta mkopo wa Tshs. 300,000, dhamana hati ya kiwanja

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Posts
3,359
Reaction score
702
Wakuu nina dharula nahitaji TZS 300,000 kwa haraka naweka dhamana hati ya kiwanja na ntarudisha TZS 330,000 tarehe 30 July 2018.
 
Kuna rafiki yangu yeye ndio mishe zake, ila kwa laki tatu unarudisha tatu na nusu, duration mwez mmoja, leta hati hyo nikupeleke ukachukue mkwanja
 
Inauma sana mtu anaomba laki tatu anatoa hati ya Kiwanja.
Hii yote ni kwa vile kila mtu anaishi kwenye mstari wa umimi ila kama ingekuwa tunaishi kwenye ujamaa tungekuwa na uwezo wa kusaidia matatizo kama haya pasipo kutoa nyaraka.
 
Hahahahaa hiyo tarehe 30 July hope hutegemei salary
 
Wakuu nina dharula nahitaji TZS 300,000 kwa haraka naweka dhamana hati ya kiwanja na ntarudisha TZS 330,000 tarehe 30 July 2018.
Duh pole sana mkuu. Kama hujafanikiwa ni PM
 
Weka maelezo ya kutosha na ushahidi wa kweli ili tukusaidie kama kweli una shida ambayo ni ya maendeleo.
Sipendi kukopesha kwa riba wala sipendi kusikia mwenzangu ana shida kiasi ya kufikia kuacha hati yake.
Sitaki ufikie huko omba msaada utakapofikia mimi najitolea 30 kwanza lakini fanya mchakato kwa wengine halafu unambie kama watakubali.
 
Hii yote ni kwa vile kila mtu anaishi kwenye mstari wa umimi ila kama ingekuwa tunaishi kwenye ujamaa tungekuwa na uwezo wa kusaidia matatizo kama haya pasipo kutoa nyaraka.
ila mkubwa hawa waomba mikopo huwa wanakuja sana na adabu wakiwa na shida. Subiri wakati wa kulipa yaanio hata kama mlikuwa marafiki urafiki wenu waweza kufa. Yaani unamuamini mtu wala huchukui collateral yoyote halafu mtu anaamua kuku abuse. Ukishapitia kitu cha namna hii unaacha kabisa kukopesha watu bila collateral. Unakuta hela ulikuwa una kazi nayo nyingine ile umemsaidia mtu sababu umeona ana shida lakini yeye anaamua kukuchukulia poa. Kwa hiyo wacha tuwe tu na roho mbaya maana binadamu hawana shukrani wala wema.
 
Na ndio maana mimi nilishakataa kukopesha ila kusaidia niko na mtu bega kwa bega.
 
Mkuu nipm tuongee kitu muhimu sana
 
Back
Top Bottom