Pia Nilishawahi kuyatangaza hapa jf haya magari lakini kama alivyosema Danniair utani mwingi hapa jf so niweka hii link ili uona na aina ya magari kwa picha zaidi.
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo-hot-deals/118527-subaru-forester-car-for-sale-7mil.html.
Hiyo Link hapo juu ni subaru.
Na hii hapa chini ni ya Freelender
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo-hot-deals/100963-car-4sale.html
Mchanganua mzima wa Biashara upo hivi
Mimi ninahitaji ushauri hata utaalamu wa kujiajiri mwenyewe nimeshafanya kazi katika makampuni mbalimbali based on project work na kwasasa sina ajira ila nilijaribu kuzunguka uku na kule nikapata mtu ambaye atakayeweza kunipa basi jipya la abiria na linauwezo wa kuchukua abiria 50-60 na tulikaa chini tukafanya mahesabu.
1. Ni africarier mwenye kuuza mabasi aina ya Eicher
2. Mkataba ni miezi 18 kulipa, Warranty 1yr, Service 6month kwake
3. Kila mwezi natakiwa nimpelekee 1M, na kila siku lazma lilaze 100,000 achilia mbali mafuta na hela ya driver na msaidizi wake,so kwa mwezi utakuta unapata 3M hapo utaona nikiwa namlipa kila mwezi according to mkataba wa 1M nitabakiwa na 2M ukitoa other charges ninaweza kubakiwa na 1.5M or 1M
Requirement
Anataka nimpatie 10M na nimwachie gari yangu aina ya Subaru forester ambayo tulikubaliana kwa sh 6.5M so total 19.5M ili anipatie basi la abiria. basi lenyewe anauza 53M ukitoa 19.5M deni litabaki 33.5M ambapo tulikubaliana ninaweza kulipa kati ya miezi 18 or zaidi.
sasa basi mimi nataka ushauri wenu nitaweza wapi kupata hizo 10M either kwa mkopo wenye riba nafuu au usiokuwa na riba ili niweze kujikwamua kwenye hali hii ngumu na ili niweze kuwa mjasiriamali?
Uhalali wa huo mkopo naoutaka ni kama nishaweka wazi kuwa kuna gari mbili kati ya moja ndio tunaweza kuweka bond or kama si magari basi hati yangu ya kiwanja kilichopo mbweni beach.
Sheria zitazingatiwa ambapo pia nitamshirikisha mwanasheria wangu na wako pia ili kuweka vitu sawa.
Lengo ni kuwa mjasiriamali na wala sio vinginevyo.
Natanguliza shukrani zangu kwa wote mlitoa michango yenu kwangu.