Natafuta mme wa kunioa

Mie ni msichana na umri wa 23 pia nina mtoto mmoja ana miezi 6, nimezalishwa tu na mtu alonizalisha hanitaki na isitoshe ameoa mwanamke mwingine. Kwa hiyo atakae kuwa tayari kunioa na tuishi kwa amani nipo tayari.
Bashite kasema mliotelekezwa wote muende kwake awape huduma, changamkia fursa binti,[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naona kama umepanic,tuliza kwanza akili then mambo yatakuwa poa tu
 
Na huyo mwanamme atanyonya nini waksti unanyonyesha. Au unatafuta kwa kukusaidia matunzo baada ya kuachwa. Ila bado una option ya kumuona Makonda.
 
Majina mazuri [emoji16][emoji16][emoji16] lakini sina imani na nyie ..nawashangaa wadada wa JF kila mmoja anajiita beautiful hahaaaa wekeni sura zenu ..
 
Mie ni msichana na umri wa 23 pia nina mtoto mmoja ana miezi 6, nimezalishwa tu na mtu alonizalisha hanitaki na isitoshe ameoa mwanamke mwingine. Kwa hiyo atakae kuwa tayari kunioa na tuishi kwa amani nipo tayari.
Binti mume hatafutwi kama bidhaa fulani sokoni. Najua umechanganywa na yule mwanamume wa kwanza. Kama walivyoshauri wengine tulia, fanya kazi zako. Mwanaume wa kukuoa atajitòkeza. Usifanye haraka. Pia humu JF sio mahali muafaka pa kupata mume. Wengi humu ni wajanja sana na wajuaji. Mume utapata nje ya JF.
 
Dah....Acha uongo bana.... Mbona Demiss kapata humuhumu JF ..[emoji13]
 
Sasa sitaki kuwateta watu waliooana humu. Wewe niambie kweli ukitaka mume ama mke ndivyo anavyotafutwa?
Dah....hakuna njia maalum ya kutafuta mke au Mume......Dunia nzima..... Cha msingi mnaendana? Baasi[emoji13]
 
Dah....hakuna njia maalum ya kutafuta mke au Mume......Dunia nzima..... Cha msingi mnaendana? Baasi[emoji13]
Ni kweli ila humu JF mimi siamini kwamba utapata mke ama mume kirahisi. Ila tukubaliane inawezekana. Isipokuwa itabidi mhusika afanye uchunguzi sana.
 
Mdogo angu,kama ungeachana kwanza na mambo ya kuolewa hivi,japo ni mambo yako binafsi na ni maamuzi yako,naona unge-focus kumkuza mwanao kwanza akitengemaa ndio mengine yafuate.....
We wa kwako ana umri gani sasa? Au bado umefunga nyonga?
 
Naona huwezi kuhandle stress,,,,


Wahi kwa Mh.Makondo kabla ya Maandamano kutokea,,

Pole sana binti.
 
Reactions: sab
Mlee kwanza mtoto akue japo afikishe miaka miwili halafu ndio uanze kutafuta mume wa kukuoa.

Wakati huo natafuta mume jitahidi ujishughulishe na kazi yoyote ili uweze kupata cha kukizi mahitaji ya kila siku
Nimependa Jina na Avarta!
 
Mmeangalia mtafuta mume ameonekana mara ya mwisho lini humu kilingeni?! Atakuwa keshampata baba mlezi wa mwana kachanga!
 

Attachments

  • Screenshot 2018-04-24 12.32.31.png
    82.7 KB · Views: 55
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…