sure steveD some common level of understanding is vital BUT not mandatory. Ila kwenye maelewano ya dhati you can agree to understand each other's deficiency na kujaribu kuyasolve.
Ila ninashangazwa na wimbi la kina dada kutafuta wachumba via internet, Nachelea kuamini kama ni kweli kwa dhati wamedhamiria hivyo ama la. kwani kwa desturi halisi za mwafrika Na feminine nature ilivyo mwanamke/msichana hufuatwa, na tena sio na mtu mmoja. Msichana ni mtu wa soni, ambaye moyo wake u tayari kupokea na kutoa upendo. They are meant to be the prey not predators.
Unajua dadangu sisi waafrika akitokea mtu humu akasema amekudondokea mkakubaliana yaweza tokea siku kaogomvi kagodo tu akakubadilikia ooh si ulijitongozesha mwenyewe! na hilo si litakuwa tusi sana?
Ushauri wangu dada, Kama imani yako ikutumavyo kuwa una imani mumeo atakuwa na vigezo hivyo (umri na masters) basi endelea kumwomba Mungu wako ukutane na huyo mume kwa njia nzuri ambazo hazitadhihirisha kuwa wewe ndio mtongozaji? Mazingira yote ya elimu, nyumbani, sehemu za ibada, michezo, safari, mikutano kweli dadangu hamna mwenye uelekeo? nina imani ukifungua macho yako ya ndani wapo. Ila kama yote yalishindikana basi Internet iwe very Last option.
Kila la Kheri tafadhali angalia sana na watakaojitokeza, si kila awindaye ni simba dada.