Mahitaji
*Iliki iliyo sagwa vizuri.
*Karot
*Hoho
*supergeti
*chumvi au sukari
Upishi
Chukua supergeti zako zivunje mara mbili, tia kwenye sufuria lenye maji, chemsha tambi zako bila kuweka chochote. Hakikisha zisiive sana maana zitakuwa laini sana endapo zikiiva sana.
*then baada ya kuzichemsha, zichuje tambi zako kuondoa maji.
*Kariti na hoho zikatekate vipande vidogo vidogo sana
Chukua chombo cha kupikia tambi zako weka jikoni, kikishapata moto, weka mafuta kiasi,
*Then weka karot na hoho, zikaange, then weka unga wa iliki endelea kuvikaanga.
*Baada ya hapo tumbukiza tambi zako kwenye huo mchanganyiko wa karot, hoho na iliki, koroga mchanganyiko wako ili zisigandie chini, then weka chumvi au sukari kutegemeana na unavyopenda.mi huwa naweka chumvi na sukari zinakuwa tamu balaa.
*Then baada ya kukoroga vizuri zinakuwa tayari kwa kuliwa.
Unaweza kuzila na rosti ya nyama au maini,. Pia hata kwa kunywea na chai pia ni tamu sana.