Pole sana kwa harakati za maisha na hongera pia kwa kuwa na ujasiri na kujishusha ili kuomba ushauri kwa wengine.
Kwanza kabisa una kitu ambacho kinaweza kukufanya upige hatua moja kwenda nyingine katika eneo la ufahamu, yaani akili. Kitu hiko ni ELIMU. Cha pili una VISION, hii ndo inakufanya uanze kuona mwanga wa maisha mbeleni kwako, cha TATU na cha mwisho ni kwamba upo tayari KUTOKA katika hali ya kipato cha chini.
Ngoja na mimi nikupe kaushuhuda kangu kadogo yamkini kanaweza kukupa kitu. Nimelelewa katika mazingira ya kishua kwa sehemu fulani hasa nilipokuwa Std 5 hadi Sekondar. Nikiwa Primary mzee wangu alinipeleka COMPUTER COURSE.
Nikaenda chuo na nikamaliza, nikapata kazi taasisi fulani nikawa nalipwa laki tatu na nusu kwa mwezi. Familia ikayumba sana kiuchumi, ikayumba sana saana. Ile kazi ikasitishwa, tukaondolewa wengi pale kazini. Nikarudi mtaani, nikaanza maisha ya kuungaunga.
Baada ya miaka kadhaa nikaanza kazi zinazohusiana na IT huku mimi nikiwa na maarifa ya Computer programs tu tena zile Basics and simple. Baada ya kuanza kazi hizi kwa kujiajiri, ndani ya miaka miwili NIKAACHANA KABISA NA KUFATILIA AJIRA POPOTE PALE. Siku moja nikakaa na mzee akasema hizi kazi ungeanza toka ukiwa mdogo hadi sasa ungekuwa mbali sana saaana.
Sasa sikiliza mkuu, ni kweli umesoma iwe CERTIFICATE, DIPLOMA au DEGREE. Hivyo vyeti vinatusaidia kupanua tu akili zetu na tuweze kuelewa mambo kwa urahisi na kuona mbali, na ili kufanikiwa kimaisha yamkini ikakupasa UTOKE katika fikra za elimu uliyosomea na kuna muda ukiona AJIRA kwako kila ukipambana unafeli, kaa chini OMBA MUNGU kuna mlango wako Mungu ameshaufungua ila ni wewe ndo umekalia kubisha mlango mmoja wa AJIRA/TAALUMA ULIYOSOMEA.
Ikiwa ndani ya nafsi yako una VISION na ni PASSION yako kufika mbali katika UDEREVA, TRUST ME UTAFIKA HUKO. Hawa akina ELON MUSK, BAKHRESA, MO nk wote hawa walikuwa na VISION zao na wakawa na passion ya kutaka kufika mbali kwa kile wanachoamini. SO, tazama vyeti vya LESENI yako, Piga GOTI MWAMBIE MUNGU KUPITIA FANI HII YA UDEREVA UTANIFAKISHA KTK MAONO YANGU. Baada ya hapo chukua hatua mdogo wangu, jikusanye nenda katafute hiyo kazi ya kusaidia udereva wa trucks, JITAHIDI upate hiyo kazi ya usaidizi na ujue utanufaika vipi kisha ndio UACHE hapo unapofanya. Baada ya hapo nenda kasome katafute hiyo LESENI KUBWA.
Wewe tayari una VISION na una mwanga so unahitaji UJASIRI na MAAMUZI ya kuvuka hapo, kuna mahali familia haitakuelewa ila simama katika vision yako sababu wewe bado ni mdogo, haujafika hata thelathini so una muda wa kurekebisha tena makosa yako. Mimi naanza hizi kazi nnazofanya sasa baada ya kukosa ajira, familia na watu wakaribu waliniona ni kama najipapatua tu ILA LEO HII KILA MMOJA ANAONGEA NA MM KWA HESHIMA, unajua kwanini? NILIONA KUPITIA HIKI NINACHOFANYA NINAWEZA KUFANIKIWA BASI NILICHUKUA MAAMUZI YA KUFANYA na by that time nilikuwa na umri huuhuu wa kwako.
NAKUTAKIA BARAKA NA KILA LA HERI UFANIKIWE MKUU.
Mwisho kabisa nilitaka kusahau, upatacho chochote iwe kidogo ama kikubwa, haijarishi wazazi wake wameacha au wapo pamoja, umegombana nao au hujagombana nao, wana ela au hawana, USISAHAU KUWAPA CHOCHOTE HATA KIDOGO UNACHOPATA, hata elfku kumi kumi wewe wape.
ASANTE.