Natafuta mtaalam wa kutengeneza LED Name Display

Quemu

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2007
Posts
984
Reaction score
133
LED – Lighting Emitting Diode

Natafuta mtaalam nyumbani wa kunitengenezea LED Name Display. Nahitaji name diplay 2 zenye ukubwa wa kama 60 x 12 (inches).

Katika ku-google kwangu nimekutana na vifaa hivi ambavyo vinatakiwa:

Diffused LEDs
Microcontroller
Serial socket
Ohm resistor
Multicore wires

Kama kuna mtaalam, basi naomba tuwasiliane. Mimi nitaweza ku-supply hivyo vifaa na vingine vinavyohitajika. Halafu tukakubaliana malipo ya utengenezaji tu.
 
Upo wapi mkuu ili tuchangamkie hiyo tenda?.
 
Upo wapi mkuu ili tuchangamkie hiyo tenda?.

Sasa hivi nimekuja mara moja kwa Obama. Lakini nitarudi Bongo mwanzoni mwa January.

Nafikiri mtu mwenye electrical engineering degree anaweza akacheza na hii kitu. Kwa sababu project hii ina involve some programming language inayohusu mambo ya Binary Codes or something similar
 
ndugu hiyo ni ELECTRONICS ,ukimpata mtu anayejua programmabla logic controller ndo hasa....
 
ndugu hiyo ni ELECTRONICS ,ukimpata mtu anayejua programmabla logic controller ndo hasa....

Sawa sawa. Je wajua mtu/kampuni inayoweza kucheza na hii kitu?
 
Sawa sawa. Je wajua mtu/kampuni inayoweza kucheza na hii kitu?

mbona vijana wa DIT wanacheza na hivyo vitu??, bongo siku hizi kila wataalam tunao, RUDINI tu homu tujenge nchi!!.
 
Mcheki Bluray...anajua kila kitu yule

Yeah...Bluray ni kama "spana-malaya"....inafungua kila kitu. Tatizo yeye anapiga boksi kwa Obama. Nami natafuta mtu ambaye yuko bongo anifanyie hii kazi.

Ningeweza kupata wataalam wa kuitengeneza hii kitu huku kwa Obama mara moja. Tatizo kuisafirisha itakuwa zoezi (60x12 inches si mchezo). Kwa hiyo ndio maana natafuta fundi nyumbani.
 
mbona vijana wa DIT wanacheza na hivyo vitu??, bongo siku hizi kila wataalam tunao, RUDINI tu homu tujenge nchi!!.

Mbona natafuta fundi aliyeko bongo ili anitengezee hiyo kitu kwa ajili ya matumizi ya huko nyumbani. Au unazungumzia nyumbani wapi tena?

DIT ndio kina nani? Una information zao (simu, website)?
 
Jamani natafuta mtaalam wa kutengeneza kitu kama hiki:

Jaribu UD...kuna wanafunzi na wakufunzi wa electrical engineering wanaweza wakakusaidia sana..
 
Mbona natafuta fundi aliyeko bongo ili anitengezee hiyo kitu kwa ajili ya matumizi ya huko nyumbani. Au unazungumzia nyumbani wapi tena?

DIT ndio kina nani? Una information zao (simu, website)?

DIT ni vijana wa Dar es salaam Institute of Technology. nasikia ila sina uhakika kwamba hata zile taa za kuongozea magari za pale bamaga sinza vijana walifanya mambo.
 
Kwa nini usinunue tu? Mbona zipo zimejaa kibao madukani.

Size ninayoitaka ni kubwa mno kuinunua huku na kusafirisha. Najua kuwa hizo size ndogo ndogo zimejaa hata ebay.

Hilo wazo la kuwacheck wanafunzi wa UD nitalifanyia kazi
 
DIT ni vijana wa Dar es salaam Institute of Technology. nasikia ila sina uhakika kwamba hata zile taa za kuongozea magari za pale bamaga sinza vijana walifanya mambo.

Yeah...hawa jamaa wanaweza wakacheza na hii tech. Ahsante GP
 
Bahati mbaya mimi nipo huku napiga box, ntajaribu kukuunganishia vijana kule bongo.
 
Unajua kusema ukweli kuitengeza hiyo kitu wala sio ngumu vile. Nikitulia hata mimi mwenyewe naweza isuka.

Vifaa vya kutengeneza hiyo kitu vipo store za vifaa vya umeme kama digikey.com. Tena wala sio bei mbaya.

Na vifaa vikishakusanywa, mchezo unabaki ni kufanya soldering ya socket board, kama hii hapo chini:

Of course, mtihani mkubwa utakuwepo kwenye kuandika program (BCD-Binary Code Decimals). Uzuri ni kwamba hata hiyo program unaweza ukaikoteza kwenye internet. Si unajua siku hizi unaweza kutengeneza hata ndege kwa kutumia internet.

Tatizo mimi itanichukua karne kuitengeneza. Electrical engineer anaweza kuifanya hii kazi kwa kutumia theluthi ya muda nitakaoutumia mimi kuifanya. Kwa kuwa sina background yoyote ya umeme and the like.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…