mwanaume halalamikiHabari za wakati ndugu zangu, Poleni sana na mahagaiko katika upambanaji wenu , wakuu
Niende kwenye mada yangu natafuta mtaalam wa Saikolojia ushauri nasaha wanapatikana wapi? Maana napitia magumu sana wakati huu mbele sioni naona Giza tu sielewi
Kazi Sina, elimu nimeishia la saba, mausiano nayo yanarega rega usiku nikilala jasho mwili mzima natetemeka nawaza mengi, Mimi bado kijana naona sielewi,
Naogopa kwenda kupima maradhi nisije nikawa nayo maana naogopa, sana 😢
Mkuu @Ushimeni kazi uliniambia Sina nauli mpaka leo nimekosa, nimeweka simu imeshindikana naomba bado kama nafasi ipo uniachie bado nijichage, kazi Sina nakuwa n mawazo sana kweli
Anataka apewe nauli😎Kuna kazi nyingine ya kuangalia shamba la mkonge Handeni Tanga huko.
Unaweza ukaenda na mkeo ama mpenzi wako na mtapewa nyumba ya kuishi.
Chakula sio uhakika sana ila nikama utapewa mlo wa mwezi 50%
Mshahara kule ni 200,000
Lakini kama hauna kamazi na unania ya kwenda kujitafutia, pana mfaa kijana kama wewe maana unaweza anzisha ufugaji wa kuku na ukajipatia amana.
Inasikitisha sana mkuu....Anataka apewe nauli😎
Nilikupa maelekezo ya kazi nakumbuka, ila niseme tu haupo siriaz na kazi mkuu.
Kama ingekua mimi ndio wewe, ningeuza sim na nikafika kwenye kazi nilio itiwa.
Kimsingi nakuona unashida iliyo anzia mbali na shida yako kubwa sio kazi, bali nakuona kama wewe ni aina ya wale watu wanaopenda kulalamika na aina ya watu kama wewe hua hawachukui hatua.
Uza sim na upate nauli ya kufika kwenye kazi nilio kuelekeza, kisha baada ya kufika basi mengine tutayatatua kwakua utakua umeonyesha nia.