Mkuu, msumbiji Provence gani ulio iona inalipa sana bidhaa kama hizo? wananchi wa msumbiji kwa asilimia kubwa wanakipato cha chini sana ingawa hela yao iko juu, na hivyo uwezo wa kununua vitu vya bei sana ni mdogo. sehemu ambayo unaweza kuuza vitu angalau kwa bei sana na kupiga hela ni sehemu ambako kunatoka madini ya mawe MONTOPWEZI provence ya kabdrigado ni hii ni kwasbb pia kuna wabongo sana .
Mimi nimekaa sana provence zifautazo Provence ya kabdrigado nimeishi Pemba, silva makua, msimbwa, mueda na montopwezi. maisha ni kawaida tu wamakuwa na wamakonde wachache wana maisha ya juu.
Provence ya Nampula kumejaa wasomali na watanzania wauza vitenge sana pale kwenye soko liitwalo bombelo, hapo pia angalau kidogo lakini maisha ya wananchi wamakuwa na wamakonde bado ni ya chini sana. ila wana penda starehe.kulewa sana, omor (LOVE) nyingi.
Nimekaa provence ya manica sehemu moja itwayo shimoyo na susundenga uko wanatumia vitu vingi vya Malawi, na Zimbabwe ni vingi sana na pia provence ya tete kwa kuwa ni majirani wanategemea vitu vya Malawi na Zambia sana,
Nimekaa provence ya sofara kule vita kila mala yule bwana JAKAMA wa chama cha Lenamo anawatwanga sana watu wa Chama Frelimo (chama tawala) kule kuna dhahabu sana ila kwasbb ya vurugu za jakama hakufai, kule beira kuna bandali ya kimataifa vitu vyao vinatoka nje moja kwa moja.
Nimekaa provence ya Maputo cidade kule yaani maitaji yao mengi wanatoa south Africa na swazland kwasbb ni karibu sana. Nimekaa provice ya inhumbane na provence quilimani huko ni kilimo kwa sana. Generaly kitu ambacho nimekigundua kinaongoza msumbiji nzima. ni starehe sana pombe kwa wingi apo utawapata waleno weusi kweli kweli. Mkuu ni msumbiji gani ambako hivyo vitu vinaenda sana?