Natafuta mtu mwenye biashara tufanye biashara pamoja

waukweli100

Senior Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
193
Reaction score
24
Kwa wale wanaotoa bidhaa China au popote duniani, iwe nguo aina zote, viatu nk naombeni mmoja wenu atakaeniamini tufanye nae biashara,mi ni mwenyeji sana nchini Msumbiji, bidhaa toka Tanzania zinahitajika, Kama hutojali nicheck kupitia 0718375766
 
Mkuu ungefunguka zaidi labda...........bidhaa gani haswa zinahitajika msumbiji?
 
Mkuu ungefunguka zaidi labda...........bidhaa gani haswa zinahitajika msumbiji?

Nguo , viatu, hivi vitenge vya wax, nasikia vina bei kweli na madira watu wanapiga kimya kimya mamilioni kuja kuzinduka weshakuwa mamilionea jaribuni kufanya uchunguzi wale wachina wakiokuwa nyomi kariakoo wamepungua sana wengi wameenda msumbiji kuwekeza.
 


Aiseee! Asante sana kwa taarifa ndugu yangu, wacha nianze mchakato.
 

kaka mimi ningeshauri kama unataka kuwekeza msumbiji dili na vyakula ila nguo sijui vipodoz bora kwetu. mimi nilikuwa pemba, hakuna move kivile ingawa bei iko juu, nilikuja kuduwazwa nilipofika mbeya mjini kitenge nilichokua nauza mimi mts. 800 mbeya wanauza 38000 wakat utofauti wa 2000 kumbuka mimi nalipia import tax wa mbeya halipi. habar ya mjini ni congo kataeeni kubali. nilikuwa najiuliza kwanini wakenya sio wengi sana nikaja gundua hakuna movement na wengi walikuwa nampula wakideal na nguo wako sasa hiv kariakoo. kiukweli nimekuja gundua zaman watu walimeki sabab wazawa wenyewe walikuwa wamelala. sasa hiv kama unaweza wekeza kwenye chakula na gest houses ni utakuwa billionea ila nazungumzia kwa mikoa ya juuu. kiukweli kwa msumbiji ukitaka win fasta usiende kwa kuambiwa stor kijiweni nenda mwenyewe. hta ukiongea na goodone(wang) pamoja ya kuwa kawekeza sana kwenye magogo pemba lkn hahami dar sabab kuna movement. ndo maaana nimesema habar ya mjin sasa hiv congo
 

congo drc au kongo kariakoo mkuu?
 
Mkuu, msumbiji Provence gani ulio iona inalipa sana bidhaa kama hizo? wananchi wa msumbiji kwa asilimia kubwa wanakipato cha chini sana ingawa hela yao iko juu, na hivyo uwezo wa kununua vitu vya bei sana ni mdogo. sehemu ambayo unaweza kuuza vitu angalau kwa bei sana na kupiga hela ni sehemu ambako kunatoka madini ya mawe MONTOPWEZI provence ya kabdrigado ni hii ni kwasbb pia kuna wabongo sana .

Mimi nimekaa sana provence zifautazo Provence ya kabdrigado nimeishi Pemba, silva makua, msimbwa, mueda na montopwezi. maisha ni kawaida tu wamakuwa na wamakonde wachache wana maisha ya juu.

Provence ya Nampula kumejaa wasomali na watanzania wauza vitenge sana pale kwenye soko liitwalo bombelo, hapo pia angalau kidogo lakini maisha ya wananchi wamakuwa na wamakonde bado ni ya chini sana. ila wana penda starehe.kulewa sana, omor (LOVE) nyingi.

Nimekaa provence ya manica sehemu moja itwayo shimoyo na susundenga uko wanatumia vitu vingi vya Malawi, na Zimbabwe ni vingi sana na pia provence ya tete kwa kuwa ni majirani wanategemea vitu vya Malawi na Zambia sana,

Nimekaa provence ya sofara kule vita kila mala yule bwana JAKAMA wa chama cha Lenamo anawatwanga sana watu wa Chama Frelimo (chama tawala) kule kuna dhahabu sana ila kwasbb ya vurugu za jakama hakufai, kule beira kuna bandali ya kimataifa vitu vyao vinatoka nje moja kwa moja.

Nimekaa provence ya Maputo cidade kule yaani maitaji yao mengi wanatoa south Africa na swazland kwasbb ni karibu sana. Nimekaa provice ya inhumbane na provence quilimani huko ni kilimo kwa sana. Generaly kitu ambacho nimekigundua kinaongoza msumbiji nzima. ni starehe sana pombe kwa wingi apo utawapata waleno weusi kweli kweli. Mkuu ni msumbiji gani ambako hivyo vitu vinaenda sana?
 
congo drc au kongo kariakoo mkuu?
Mkuu nakubariana na wewe kabisa yaani mimi msumbiji kwakweli naijua kiasi flani hata kileno chao nakijua kushinda kingeleza, ila sasa katika nguo duuu sijui lakini. ila kwenye starehe, guest house apo utawapata sana. guest house ni tatizo sana msumbiji hakuna za kisasa. lakini pia pombe utafikiri wali laaniwa mkuu!!! Mimi nimeishi sana Maputo ukienda soko la wajanja waputo liitwalo estrela mericado, utakuta pombe za aina yote na ikifika ijumaa duuu mwnawane kila mtu na wake, kwakweli. na pia haki za binadam bado hazijaweka sawa kwa msumbiji. police kwa kuwa wana kasumba muda wowote wanakagua id (Birrihet or passapot) akiamua kukubambikiza ishu isee unalo mpaka utoe mitikash ya kweli. kama uko congo sipajui vizuri ila kama kuko poa ni vema watu waelekeze nguvu uko,
 
Biashara ya transportation vipi? Kusafirisha mizigo, makontena etc.
 

Kaka Felix inaonekana Msumbiji unaijua vizuri sana
 
Biashara ya transportation vipi? Kusafirisha mizigo, makontena etc.

Biashara ya usafirishaji unaweza kupata mkuu. watanzania wakubwa wanao fanya biashara hizi za usafirishaji msumbiji ni mwarabu mmoja anakampuni iitwayo NAGE IVESTMENT ila ni mtanzania, na mwingi ni huyu maningi nice ambaye naye ni mtanzania. na wewe una weza kufanya mkuu
 
Asante. Wewe bado unaishi msumbiji au umesharudi bongo?

 
Asante. Wewe bado unaishi msumbiji au umesharudi bongo?

niko Tanzania kwa sasa nina wiki 2 mbili nimerudi, nitanda tena tarehe 15 mwezi huu.ila nitaenda kule MANASHA
 
kwa mkoa ambao nilikuwepo mm ni mkoa wa nyasa sehemu flani inaitwa lichinga ni mkoa ambao umepakana na malawi,vitu ambavyo vinauzika kule ni viatu,vitenge,nguo kama surual,tshert,na pia za kike,mi kaka yangu yupo mpaka leo huko anapiga kazi huwa anakuja tz kuchukua mzigo.
 
niko Tanzania kwa sasa nina wiki 2 mbili nimerudi, nitanda tena tarehe 15 mwezi huu.ila nitaenda kule MANASHA

Madini ya ruby yanapatikana kwa wingi province ipi??
 
acha nikujibu mm maana naona mkuu felix katiririka vya kutosha, wilaya ya mptopwez kuna sehemu inaitwa nyanupu hapo ndy ruby ipo

Je msingi wa kuanzia kununua ruby kama tshs ngapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…