Natafuta mtu wa kuwekeza kwenye nyumba kutoka Makazi binafsi kuwa ya Makazi na Biashara

Natafuta mtu wa kuwekeza kwenye nyumba kutoka Makazi binafsi kuwa ya Makazi na Biashara

Qifrishy

Senior Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
169
Reaction score
42
Habari wakuu.

Nyumba hii ipo maeneo ya sinza kijiweni ni dk 1 kutoka barabarani (hayo ni makadirio ya juu), ipo mkabala na Habari House. Nyumba ina documents zote za kiserikali. Kwa sasa nyumba hii ni ya makazi binafsi. Natafuta muwekezaji wa kuibadili kutoka kuwa nyumba ya makazi binafsi kwenda kua ya kibiashara.

Mpango wenyewe ni kujenga Fremu za maduka kwa na kuweka makazi ya watu hapo hapo. Eneo husika linaweza jengwa gorofa ambalo chini kutakua ni fremu na juu kuweka apartments kwa ajili ya makazi ya watu ambao wata pangishwa kwa malipo ambayo yatawekwa hapo baadae.

Mimi ninae andika ndo muhusika na msimamizi wa eneo lengo haswa hapa ni kua pakishwa jengwa eneo la makazi ya kibiasahara mimi nabakiwa na umiliki wa eneo na usimamiz wa eneo husika na pia kupewa apartment mojawapo kwa ajili makazi yangu na familia yangu.

Ila pia kwenye swala la usimamizi wa eneo haswa upande wa kibiashara tunaweza shirikiana na muwekezaji husika. Mapato ya faida nzima ya biashara yatagawanywa kwa makubaliano baina yangu na muwekezaji.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia.
0655220039
0654687403
 
Naitamani sana hiyo fursa ila kwa sasa mtaji wa kutosha hiyo kwa sasa sina, subiri Wakinga waje hapa waichangamkie. Ila ni kwanini usiende bank au taasisi yyt ya kifedha inayotoa mortgages
 
Back
Top Bottom