jamani mi natafuta mwanasaikologia wa kunisaidia kuondokana na woga kwani nina tatizo hilo hadi nashindwa kabisa kuongea mbele ya watu,,,,hivyo nimeshauriwa na rafiki zangu nitafute mwanasaikolojia kwani tatizo langu litaweza kupungua na hadi kuisha kabisa, hivyo naomba mnielekeze kwa hao wanasaikolojia wanaopatikana jijini dar kwani nitakuwa huko mwezi huu mungu akijalia uzima. asanteni
jarbio la kwanza naomba utumie jina lako halisi hapa jamiiforum, acha kuzuga na diet, ukifaulu hapo nakupa test ingine mpaka uwe na uso wa mbuzi
Wakuu Kiswahili kimepanuka Mtu kuwa na Uso wa mbuzi ndi vipi jamani? Sipo siku nyingi kiswahili kimepanuka namna hivyo nielewesheni jamani wakuu wenzangu SoNotorious na charmingladyDuh... pole mkuu... ngoja wenyeji waje. Ningeweza ningekugaia uso mbuzi wangu....
Wakuu Kiswahili kimepanuka Mtu kuwa na Uso wa mbuzi ndi vipi jamani? Sipo siku nyingi kiswahili kimepanuka namna hivyo nielewesheni jamani wakuu wenzangu SoNotorious na charminglady
Mkuu SoNotorious Mmmmhhhhh umefika mbali mkuu bado hujanijibu kabisa sijaridhika na jibu lako ni nini maana ya uso wa mbuzi?kuwa na uso wa mbuzi ni kuwa kama JK, unakosa mshipa wa noma
Huu ujumbe ni kwa mtoa mada au nani?? Kama ni kwa diet utakuwa umekosea sana, kwani hujui kuwa kuwa na aibu nao ni ugonjwa??Tumefika hapa tulipo kutokana na watu kama hawa wasiojitambua na hawajui kama hawajitambui HATA OBAMA akiwa RAIS wa BONGO kwa mtindo huu bado ni zero hili ni jukwaa serious ambapo people can discuss mambo muhimu kuhusu afya zao unakurupuka tu UNASHINDWA HATA NA MIMI UNDER 17 NILIEJIUNGA JF JUZ.
Mkuu SoNotorious Mmmmhhhhh umefika mbali mkuu bado hujanijibu kabisa sijaridhika na jibu lako ni nini maana ya uso wa mbuzi?
Bibie diet Pole kwa hayo matatizo uliyokuwa nayo jaribu kutumia hii dawa yangu kula kwa wingi hii dawa inaitwa Lozi au kwa kiingereza inaitwa Almond kula kutwa mara 3 kwamuda kama mwezi mmoja kisha uje hapa kunipa feedback angalia kwenye picha Lozi inasaidia kuondowa wasiwasi na Woga na maradhi mengine tu.
Almond Lozi inapatikana Sokoni kariakoo au katika Ma-SuperMarket pia inapatikana ni Dawa ya kuondosha wasiwasi na woga na maradhi mengine.
Lozi inajulikana kama ni King katika jamii ya njugu, ina elements karibia ya zote zinazohitajika katika mwili wa mwanadam. Ni chakula chenye kutia nishati mwili na akili.
Kuna aina mbili za Lozi, kuna lozi zile tamu na kuna lozi chungu kuna zenye ngozi nyembamba (thin-skinned) na kuna zenye ngozi nene(thick-skinned) hii ni katika aina ya lozi tamu ambazo ndio tunazozitumia na tunahitajika kutumia ama zile lozi chungu zina prussic acid ambayo ni sumu hata hivo hizo lozi chungu zinatumika katika mambo ya kutengenezea cosmetics, mafuta ya lozi (almond oil) pia na perfumes.
Nchi mashuhuri yenye Lozi ni Morocco, pia lozi zilionekana katika miaka mingi nyuma katika nchi ya Syria na Palastine inasemekana katika zama za Nabii Issa A.S. Hata hivo sasa hivi lozi zinazalishwa sehemu nyingi duniani kama Italy,California,Australia,Sou th Africa,Kashmir na sehemu nyingi za Asia.
Food Value: Minerals and Vitamins
Moisture 5.2% Calcium 230 mg
Protein 20.8% Phosphorus 490 mg
Fat 58.9% Iron 4.5 mg
Minerals 2.9% Niacin 4.4 mg
Fibre 1.7%
Carbohydrates 10.5%
Ndani ya lozi pia kuna upatikanaji wa copper, iron phosphorus na Vitamin B, vitu hivi vinasaidia katika upatikanaji wa new blood cells, haemoglobin pia inasaidia ubongo, mishipa, mifupa, moyo na ini kufanya kazi kwa wepesi kabisa. Lozi insaidia kupanua na kutia nguvu muscles za ubongo katika kuongeza fahamu.
Old ages:Utu uzima wa kiumri.
Chukua lozi kiasi na uziroweka katika maji na baadae utoe ngozi yake ikisha uzisage na kufanya paste kwa kutumia kama siagi, hii huongeza proteins ndani ya mwili na hasa kwa watu wazima, pia unaweza kutia katika maziwa na ukanywa hii nzuri kwa watoto.
Anaemia: upungufu wa damu
Kuna upatikanaji wa copper katika lozi katika rate 1.15mg per 100 grams, copper pamoja na iron na vitamins hizi zinatumika kama ni catalyst katika mfumo wa blood haemoglobin. Kwa hiyo wenye maradhi ya upungufu wa damu ni vizuri mtu kutumia lozi kwa sana.
Constipation:kupata choo
Kwa wale wenye matatizo ya kupata choo, ni uzuri kula lozi wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala.
Impotency:upunguvu wa nguvu za kiume
Kwa wale wenye upunguvu wa nguvu za kiume na za kike, wale lozi kwa wingi.
Skin Disorder:maradhi ya ukoma
Kwa wale wenye maradhi ya ukoma, wasage lozi iwe laini ikisha wajipake pale palipoathirika, na pia kwa wale wenye pimples. Chanzo: MziziMkavu ( Specialist Researcher for herb Treatment)