Natafuta mwanamke wa kuoa nipo serious kwa hili

Natafuta mwanamke wa kuoa nipo serious kwa hili

Asante Jehovah

New Member
Joined
Jan 19, 2018
Posts
2
Reaction score
5
Hellow, najitokeza Kwa Mara ya kwanza kutafuta mke wa Kuoa.Kwajina naitwa Johnson mwenye Umri wa miaka 35,dini yangu ni mkristu (RC), rangi na muonekano wangu ni mweusi, urefu na unene niwa wastani, elimu yangu Nina shahada ya kwanza fani ya biashara.

Mke ni mtakaye awe na Umri kuanzia 24-28, Asiwe mlevi wa sigara wala pombe kupindukia. Sina ubaguzi wa dini , kabila, elimu, kazi, rangi wala muonekano wa mtu Bali nachojali awe amemaanisha kujenga familia kwa pande zote mbili.

Kwa atayekuwa tayari tuwasiliane kwa email yangu ya Jehovahnishindie@gmail.com, au ni pm tuyajenge na kufikia lengo la kuitwa wana ndoa. Kwa ataye kua anaishi mikoa hii (Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Rukwa, Katavi,) atapewa kipaumbele.

Nahitaji umakini kwa hili nipo serious utani sipendi kwani hakuna kanuni jinsi ya kumpata mke.
 
Huwezi kupata mwanamke bora ukiwa umeinyoosha miguu juu huku ukichezea keyboard za smart yako! Acha uvivu, acha uzembe ingia mtaani uchangamke! Uwe makini kumtafuta unayemwona anakufaa....ukishindwa mwambie Shangazi yako kule kijijini akutafutie mchumba na sio wa mitandaoni
 
mimi miaka yangu kama yako tu kipengere cha umri kimenikwamisha
 
unatafutaje mke mtandaoni aisee... mizunguko yako yote unataka kusema huoni au wanakutolea za mbavu..!!!!
 
Hajachelewa yupo sawa tu,hakuna shida Mungu atamsaidia.

~Nilianza mbio za kumsogeza mdogo wangu hapo nimuadilifu kweli kweli nlitaka nikutunuku ss ulipo taja tu mikoa ukaua bendiii.maana nikaona umebagua tayari.ila kila lenye heri
 
Back
Top Bottom