Natafuta Mwanamke wa kuzaa naye kisha tulee mtoto pamoja

Natafuta Mwanamke wa kuzaa naye kisha tulee mtoto pamoja

affinitytz

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2020
Posts
216
Reaction score
1,007
Wadau nafahamu watu wana mahitaji tofauti tofauti hapa. Nimeona kuna wadada/wanawake wenye uhitaji mtoto na huwa wanatafuta mtu mwenye muelekeo ili waweze kupata mtoto pamoja.

Sasa ipo hivi; Mimi ni kijana miaka 34 ; Mkristo
Elimu yangu ni Degree moja; nipo natafuta ya pili kwa sasa.
Makazi Dar es salaam.
Nina watoto wawili lakini nina uhitaji wa kuongeza mtoto mwingine.
Nimezungumza na mke wangu (yeye sio Mtanzania) na amekubali kwa kuwa yeye kwa sasa anafocus kwenye career yake na hana na haitaji mtoto mwingine.
Sasa basi tupunguziane matatizo
Kama yupo mdada/mwanamke mwenye uhitaji wa mtoto (tutamlea pamoja na nitatoa huduma zote katika malezi).
Sifa:
Dada/mwanamke
Dini: Sio kigezo (hatuji kufundishana dini wala kuswali).
Ila kama itakuwa ni Mkristo basi tutakuwa tukienda kwa ibada pamoja.

Makazi yawe Dar ili tupate muda wa kumlea mtoto pamoja. (Ni muhimu sana mtoto akikua huku akimuona baba na mama pamoja).

Umbile: Asiwe mnene sana ( sio tu kuwa mama lakini tutakuwa tukiambatana kwenye matukio mbalimbali na Mimi nina mwili wa wastani tu hivyo ili tu-match). Mabinti wanene wa wastani karibuni pia.

Asiwe mrefu sana (napenda short chasis zilizojaa vizuri). Wale wenye mwili wastani karibuni pia.

Mdada/mwanamke mwenye kuwa na tabasamu (napenda furaha).

Rangi: Maji ya kunde au mweupe kidogo.

Awe na ajira/biashara yoyote ( nakuja kuwa mzazi mwenza sihitaji senti tano yako lakini kujishughulisha ni muhimu).

Kama yupo mwenye uhitaji na sifa hizo. Karibu sana PM.

Hubebi tu mimba bali unakuwa mzazi mwenza na mpenzi wa kudumu.

Maswali na makubaliano mengine tutazungumza.

==========

Update: Tarehe 19/02/2020

Wadau, tayari nimeshapata binti mmoja wa kinyamwezi na ana sifa zote nilozokuwa nahitaji na ziada.
Nimeshakutana naye juzi usiku pale Rissa Mtaa wa Lumumba na Jana pia pale NAKOS - Kigamboni maana wote ni wakazi wa Kigamboni.

Asante kwa wale wengine waliojitokeza bila shaka ipo siku mtapata hitaji lenu.

Kwa waliohoji utayari mke wangu ni kuwa yeye ni mtu wa Sweden na anafanya kazi kwenye shirika moja wapo la Umoja wa Mataifa na kwa sasa hayupo nchini kwa miaka kadhaa.
Na hawa wenzetu wapo wazi sana anaposema anamaanisha.

Asanteni sana.

Note: JF kuna wadada warembo sana.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napenda short chasisi zilizojazia nyama za Allah... hahahhaa sheny sana we malaya tu mbona
 
Watoe hofu dada zetu weka picha wakuone isiwe kama yule tulieambiwa afanya kazi UNHR mdada wa mwanza alichokutana nacho akaja kutueleza
 
Kuna wimbo mmoja zilipendwa umecharazwa na raia wa Kenya usemao 'mtoto si nguo utaomba mtu' umenikumbusha kitu.

Hili nimelibadili kwa mke!

Hivi mke wa kuweza kulala naye, kushea naye maisha, kisha kuzaa naye, waweza kumpata kwa kupitia matangazo kama ajira?

Nadhani unatania!

Kama upo serious nadhani unamapungufu makubwa sana kichwani mwako, ndiyomaana huyo 'mdiaspora' kajiondoa kijanja!

Mila na desturi za Tz, mwanamke wa maisha hatafutagwi hivyo, labda kama unatafuta nungayembe la ku date nalo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahah usiwe mnene ili akikukumbatia mu match.

Short chasis iliyojaaa nyama kwa lugha nyingine ni yenye makalio makubwa

Au kwa bihaviourist ni enye chura kubwa.

Wahi nafasi ni chache
Kigezo cha urefu kimenikosesha mzazi mwenza, hii long chassis imenicost, kila rakheri, ila kama hata matukio mtakua mkiambatana pamoja na huo ukaribu si ni mke tayari huyo?, mkeo anazungumziaje hilo? tusije mwagiwa tindikali buree

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Update: Tarehe 19/02/2020

Wadau, tayari nimeshapata binti mmoja wa kinyamwezi na ana sifa zote nilozokuwa nahitaji na ziada.
Nimeshakutana naye juzi usiku pale Rissa Mtaa wa Lumumba na Jana pia pale NAKOS - Kigamboni maana wote ni wakazi wa Kigamboni.

Asante kwa wale wengine waliojitokeza bila shaka ipo siku mtapata hitaji lenu.

Kwa waliohoji utayari mke wangu ni kuwa yeye ni mtu wa Sweden na anafanya kazi kwenye shirika moja wapo la Umoja wa Mataifa na kwa sasa hayupo nchini kwa miaka kadhaa.
Na hawa wenzetu wapo wazi sana anaposema anamaanisha.

Asanteni sana.

Note: JF kuna wadada warembo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom