Natafuta mwanaume

Hilo nalo neno. Hata mimi kuna mmoja alifanya kitu kama hicho ila siyo hapa. Kumbe shida yake ilikua kakwama ada ya mtoto wake. Kazalishwa na wengine huko anakuja kujitangaza eti anataka mchumba kumbe nia yake ni kumvulia shida zake zote.

Dada funguka tujue!Usije ukanifanya kama yule mdada!Kaniita PM hapa tukakubaliana na uchumba ukashika kasi kumbe lengo lake lilikuwa NIMNUNULIE KING'AMUZI na alipokipata tu na simu hapokei!
 
Mnapoteza muda tu, mwenzenu anataka mwanaume siyo mume kwahiyo hapa ni kutangaza dau a.k.a mkwanja, nyie mnataka kujua wasifu wake. Naku - PM sweetie, dau langu najua huwezi kataa.
 
Dada funguka tujue!Usije ukanifanya kama yule mdada!Kaniita PM hapa tukakubaliana na uchumba ukashika kasi kumbe lengo lake lilikuwa NIMNUNULIE KING'AMUZI na alipokipata tu na simu hapokei!

tehe..tehe...tehe........... mbavu zangu mie unaniongezea njaa wangu sio vizuri kabisa
 
Ujumbe wa Jane wa
Mwenge kwa mlio lala nae


“Nimeambukiza maelfu ya watu VVU
katika jiji la Dar”
Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es
salaam naomba utalifuta jina la baba
yangu maana sitaki liwe kwenye blog
watu watanijua na kuniangamiza
maana nimeshawaangamiza wengi sana
kwa UKIMWI ila mengine yote usifute
hata moja ili dunia ijue tu japokua
mimi nitakufa kwa huu ukimwi
nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi
vizuri tu tangu utotoni na hata
sikujihusisha na ngono hadi
nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada
ya kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi
kwa mama mdogo aliyeolewa hapa
Mwenge.
Nilipata marafiki wengi tu na kuna
kijana mmoja alinitongoza kwa muda
mrefu sana na siunajua vijana wengi
hutumia muda mrefu kutongoza ili
msichana unadhani kwamba labda
huyo anakupenda kumbe anataka tu
ngono na wadada wengi sana hudhani
kufuatiliwa kwa muda mrefu na
mvulana basi huyo yuko serious
kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila
nilikataa kuhusu kufanya mapenzi
maana anayekupenda kiukweli sio
uongo lazima asitake ngono kabla ya
ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia
kuhusu kufanya mapenzi nilikataa
alitumia mbinu nyingi sana kwa
kunibembeleza na hata kulia mbele
yangu ili tufanye tu mara moja ila
nilikataa, alisema atavumilia hadi siku
ya ndoa yetu ambapo tulipanga
kuoana mwaka sept 2009.
Siku moja aliniambia twende kwenye
kumbi za starehe na mimi kwa sababu
ya upagani na kumwamini pia kwa
sababu nampenda nilikubali tulienda
huko na kulikua na bendi fulani
maarufu ya mziki wa dansi ilikua
inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi
wangu akaagiza pombe alianza kunywa
huku akinionjesha, nilikataa kwa
sababu nilikua sijawahi kunywa
pombe katika maisha yangu yote, hata
sijui alinishawishi vipi nilijikuta
nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa
tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa
5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4
japokua nilikua nakunywa kidogo
kidogo tu tena kwa kunywesha na
mpenzi wangu maana nikama nikua
nanyweshwa kila baada kama ya
dakika 25 ndipo nakunywa mara moja
na sikujuia kama nakunywa pombe ila
niliihisi tu naonja ili kumlizisha
mpenzi wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi
usingizi na pia nilijiona wa tofauti
najua nililewa hata kama sikujua
kama nimelewa maana nakumbuka
tulitoka pale huku amenishika mkono
huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax na
kuondoka na siku hiyo aliniambia
twende kwake alikokua amepanga
chumba maana tulikua na usingizi
sana nilikubali huku nikidhani
hatuwezi kufanya mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani
ukweli pombe ni kichocheo cha ngono
na ningekua mimi ndio Raisi wa
Tanzania ningefunga bar zote.
Nilijikuta natamani kufanya mapenzi
na huyu mpenzi wangu hata alikua
hana nia maana alijua atanichukiza
sana na uhusiano ungekufa siku hiyo
lakini kwa sababu ya pombe
nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo
maana mwili wangu unataka.
Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya
pombe nilifanya mapenzi na huyo
mpenzi wangu na baadae akanipeleka
nyumbani baada ya wiki mbili maana
tulikaa wiki mbili bila kuonana
alikuja na kunieleza habari ambayo
sikuihitaji katika maisha yangu maana
nilikua nasikia tu kwa watu wengine
lakini sio kwangu alisema ”JANE ISHI
KWA MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia
kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka
mitano iliyopita na anapenda tu
ngono maana hawezi kuacha.
Nililia sana na baada ya wiki moja
baadae nikaenda kupima na kukutwa
nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa
watu na chanzo cha yote ni pombe,
kupenda starehe,disko na upagani
unaotusumbua wanadamu wengi.
Nilikua na UKIMWI na kwa hasira
maana mpenzi wangu alihamia Arusha
huku akisema neno moja la mwisho
kwamba ”shetani amemtuma
kuwaambukiza wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua,
sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU
nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa
mzigo ambao haukunistahili mimi.
Hata leo hua najiuliza kwamba
nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini
pombe na huyu wakala wa shetani
wamenifanyia hivi. Baada ya kujua
nina UKIMWI na hali hiyo nikaikubali
na kulikua na kundi kubwa sana la
wanaume ambao walikua wamewahi
kunitongoja na niliwakataa sana kwa
sababu hii niliwakubali ili nami nife
na wengi.
Nilianza kumkubali kila mmoja na
kuna baba mmoja ambaye ana wake 3
niliwahi kumtukana sana kipindi cha
nyuma kila aliponitongoza lakini
wakati huu nilimkubali na hakuamini
na tukafanya ngono tena bila kinga na
akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi
ya kumkubali kumbe naye hakujua
kuwa namwambukiza na hata leo hua
nawahurumia tu wale wake zake
ambao wana UKIMWI uliotoka kwangu.
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi
1500 maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo langu
niwakomeshe kama mimi
nilivyokomeshwa na nina uhakika
kutokana na mimi wameambukizwa
UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na
hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa
linaniliza kila siku maana hata mimi
najua kabisa nilianzisha mtandao
kama huo wa ngono kwa idadi kubwa
sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku
naombewa nilikutwa na mapepo mengi
sana na hata waombeaji wakashangaa.
Ningejua ningeokoka tangu nikiwa na
miaka 5 lakini ndio hivyo sina jinsi
wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo.
Na naomba kila atakayesoma ujumbe
huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni
dhambi pia kwenda disko ni
dhambi,kuuza pombe ni dhambi na
kila kichochoe chochote cha dhambi ni
dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi
kujua kama nina UKIMWI na sijui
MUNGU ana mpango gani na mimi
maana kwake yote yanawezekana.
Nauamini uponyaji wake na sijawahi
kutumia ARV hata siku moja na afya
yangu iko sawa tu na huwezi hata
wewe kujua kama uovu huu
nimefanya mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda
kanisani ukaombewe na kama una
akili mpe YESU maisha yako maana pia
baada ya kifo ni hukumu. Yasalimishe
maisha yako kwa YESU na usiambukize
wengine tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya
mapenzi tena na sitafanya hivyo wala
sitaolewa na mtu yeyote maana
yatosha kwa uovu niliofanya na hadi
sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15
wameshafariki na nilihudhulia
misibani huku nikijua kabisa chanzo
ni mimi.
Mwisho nawashauli wababa kulidhika
na wake zao na wamama pia lidhikeni
na waume zenu, vijana ambao
hamjaoa wala kuolewa subiri hadi
utakapooa au kuolewa na kabla ya
kuolewa au kuoa kapimeni kwanza
kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko
unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani na
pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU akubariki
Ni mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
 
Na bado. Umezunguka facebook weee na kugegedwa na kuachwa na kukimbilia jf na....na...utakoma. Mabinti wengine jifunzeni sio kulinga weee wakati mnaona usiku unazidi kusonga.
 
unaweza kukuta bonge la kizee ha ha ha ndo maana unatuwekea namba feki hakuna wahuni labda fb.
 
Dada funguka tujue!Usije ukanifanya kama yule mdada!Kaniita PM hapa tukakubaliana na uchumba ukashika kasi kumbe lengo lake lilikuwa NIMNUNULIE KING'AMUZI na alipokipata tu na simu hapokei!
mmmmmmmmmmh!noma hiii!ukajiachiaa tuuh?kali hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…