Wapendwa hodi tena, nimerudi kuwashukuru wote mliochangia mada yangu hii ya kumtafuta mwenza. Imekuwa ni ajabu na kweli, yaani kama utani vile ila namshukuru Mungu. Wengi waliona natania lakini kiukweli nimepata mume humuhumu JF.
Kilichonishangaza ni kwamba amekuwa muwazi sana kwangu,amenionesha pande zote mbili za tabia kwani hakuniuliza chochote kuhusu mapenzi, badala yake alianza na suala la afya zetu, na hadi sasa hakuna nisichokijua toka kwake. Anawafahamu wazazi wangu na kuongea nao. Tumeshafanya yale ya msingi na mwisho wa mwezi huu ankuja na ndugu zake kwetu, mama yangu pia anamfurahia sana. Jamani asanteni na ningependa kuchukua nafasi hii adimu kuwashawishi na wengine wanaotafuta wenza wasikate tamaa kabisa kwani kama vile mimi nilivyopata nao watapata.
Narudia kusema asanteni sana.