Natafuta namba za simu za bajaji, tax na pikipiki mikoa yote ya Tanzania

Linda Yusufu

Member
Joined
May 3, 2018
Posts
11
Reaction score
6
Habari, naomba nisaidie waungwana nimepewa kazi nitafute kila mkoa namba za simu za bajaji, pikipiki na tax majina ya huyo dereva na anapopaki.
Dhumuni la kufanya hivi ni tukiwa na wateja wetu wanaokuja mikoani tufanye biashara tutakuwa tunawasiliana unawachukua na kuwapeleka sehemu mbalimbali

pls naombeni msaada wenu kama mnamjua yoyote.

Asante
 
Unawezaje kuomba namba za simu za watu na majina yao ilhali wewe unatumia jina la bandia !!!
 
Mkuu hata Uber hawakufanya kisanii kama unavotaka kufanya. Andaa utaratibu weka idea mezani wenyewe watakufuata. Wewe tu unaponunua bidhaa ukiombwa namba yako ya simu unawaka moto
 
Mkuu hata Uber hawakufanya kisanii kama unavotaka kufanya. Andaa utaratibu weka idea mezani wenyewe watakufuata. Wewe tu unaponunua bidhaa ukiombwa namba yako ya simu unawaka moto
thanks kwa ushauri nitalifanyia kazi
 
I see! Hii ni tresspassing mbaya sana. Unadhani ni halali kwako kuwa namba za madereva bodaboda na Bajaji nchi nzima man? Serious kabisa? Kwa nini ha wageni wako wasichukue hizo namba kwao wenyewe wenye hivyo vyombo vya moto kila wakifika huko wanakoenda?
 
Una idea nzuri ya Biashara lakini unataka uifanye kiuficho....kwa ombi lako ni una mpango wa kuanzisha App.....shirikisha wadau wazo lako utapewa njia bora za what to do,namba nchi nzima sio mchezo aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…