Uko tayari kwa:
Kuhonga nyumba jumla, gari jumla, shamba jumla na samani zote za ndani jumla kisha, mwisho wa kutembelea nyumba ndogo saa 5 usiku? Maana una nyumba kubwa utakumbushwa saa 5 usiku ukifika kuwahi nyumba kubwa vyumba visilale wazi huko. Huruhusiwi kuja nyumba ndogo bila taarifa au hodi. Matumizi kwa siku au kwa mwezi ni mara 95 ya matumizi ya nyumba kubwa, japo hiyo itakuwa ndogo. Ukishahonga vilivyotajwa hapo juu na mfuko ukalegea au ukagoma kuongeza matumizi zaidi unapigwa mkwara usepe zako utafute ndogo nyingine. Kama hayo unayaweza, sema tukuunganishe.