Jee una uzoefu na hii biashara ama ndio unaanza, mimi sina utaalamu huko lakini kuna jamaa yangu alinunua mashine kama hio kwa gharama ya milioni 10 matokeo imeharibika ndani ya miezi miwili, kwa hio ushauri wangu kama huna utaalamu na hizo mashine kabla ya kununua tafuta mtaalamu ili akupe ushauri juu ya aina gani ununuwe kulingana na ubora, uzalishaji na uimara wa hio mashine, pia unaweza kuangalia uwezekano wa kukodi jiko kwa kuanzia, mfano kama utakuwa na usafiri wa kwako na upo karibu na bekari kubwakubwa unaweza kukodi oven zao kwa masaa pengine 3 hours kila siku, hii itakuepusha na gharama za umeme, matunzo (service) ya hio oven nk.