Natafuta partner wa biashara ya samaki

Jenseny

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
1,743
Reaction score
1,738
natafuta partner wa biashara ya samaki anayeweza kufanya biashara na Mimi ya Samaki kutoka ruvu upande was Simanjiro Manyara

Sifa
awe na uzoefu wa biashara ya Samaki ayajue masoko
awe na usafiri unaoweza kubeba kuanzia Tani moja
awe tayari kuingia moja kwa moja kwenye eneo la kutafuta samaki
awe na mtaji Kama wa kwangu au ulionizidi kidogo

Upatikanaji wa Samaki

Samaki Aina ya tilapia/Sato au perege wanapatikana kwa wingi eneo linaloitwa Zambia Mazinde Hadi Remiti wilayani Simanjiro

huku wanauza kwa ndoo ndoo moja ya tilapia ni Kati ya elf 70 Hadi 80 catfish au kambale ni Kati ya elf 40 Hadi 55

mAsoko;
tunaweza kuuza kwenye mAsoko nliyozoea kupeleka samaki

Manyema
Bei za samaki sokoni Zina range Kati ya laki na 20 Hadi 90 soko likiwa baya kwa tilapia na Kati ya sh 80 Hadi 60 soko likiwa baya

Kilombero Arusha

Bei za samaki sokoni Zina range Kati ya shilingi laki na 40 Hadi 90 soko likiwa baya kwa tilapia na Kati ya sh 80 Hadi 70 kwa kambale

kuuza kwa kg
ndoo moja ya sato au tilapia Ina kg 18kila kilo moja ni sh 7000 ukiuza kwa kilo unapata avarage ya 130000 kwa kila ndoo ya tilapia na ndoo ya kambale Ina kilo 20 kila kilo no sh 3800 ukiuza kwa kilo kila ndoo unapata 76000
changamoto ya kuuza kwa kilo no kupata mteja was kununua kg zote na kukulipa kwa cash wengi wanaopenda kukopa
kwann tufanye biashara ya samaki

ni biashara ambayo ipo real ukinunua ukifungasha ukisafirisha unajua ushakua unapata faida gani na kwa muda gani

ni biashara ambayo ukiwa nje unaweza kuwaona watu ni wajinga wanuka shombo lkn ukiingia ndani ya field Kama una mtaji nlokutajia hapo juu utapata faida haraka zaidi ya biashara yoyote


kwann nahitaji partner
niliiibiiwa mtaji Kati ya mwezi wa 8 na 9 hivyo nimeshindwa kurudi kwenye pick Kama nlivyokua mwanzoni

mawasiliano nicheki dm
 
Kiasi gani cha mtaji
 
Naomba nitafute kwa namba 0673222450 tuwasiliane kibiashara zaidi
Nicheki kwa namba 0673222450 tuwasiliane zaidi ki biashara
 
Nitafute tufanye biashara 0673222450
 
Naomba kujua hii biashara zaidi Nicheki kwa number 0673222450 au Nitumie namba yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…