Natafuta partner wa kufanya naye biashara ya ufuta

konabar

Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
25
Reaction score
19
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, naishi Rufiji Bungu, ni eneo linalojishughulisha sana na shughuli za kilimo hasa mihogo, ufuta na korosho. kipindi hiki ni kipindi ambacho ufuta unavunwa kwahiyo wakulima wanauza ufuta kwa watu wenye mitaji kwa tsh 2000/= kwa kilo na Serikali inatarajia kununua kwa 3500 kwa kilo. Nakaribisha mtu yeyote mwenye cash na kutaka kutengeneza faida ya 1500 kwenye kila 2000/=. na prefer kwa waliokaribu hasa maeneo ya Dar.

Ili uweze kuona nini kinanunuliwa at list kila week na kuepusha lawama na kukiona kinachonunuliwa bila kusahau lile zao jingine la mwezi wa 9 tunaweza shirikiana na kuliuza bila shida...... kwa yeyote atakaependezewa anicheki inbox. Kuna watu tumezungukwa na fursa lakini hatuna mtaji na kuna watu mna mitaji lakini hamna fursa au mnabanwa na kazi za kuajiriwa, tushirikiane kujikwamua kiuchumi, amina.
 
Bila mawasiliano? Na je selikali isipo nunua au ikinunua kama ilivyonunua korosho?
 
Bungu ni kibiti kiongozi sio Rufiji... Nilishituka nikadhani upo Rufiji tupige kazi... Karibu Nyamwage Muhoro Miwaga...
 
Hii siyo kangomba mkuu? isije ikawa shida kama iliyotokea kwenye korosho
 
Duh! Huko kwenu ufuta haupo under control ya vyama vya ushirika? Maana nanusa harufu ya kangomba hapa[emoji16]
 
Serikali ya nchi gani inakuja kununua ufuta na ni lini? Acha kudanganya watu wewe.

Tarehe 1/June >Waziri akiri mkanganyiko soko la ufuta. WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, amekiri kuwapo mkanganyiko katika ununuzi wa zao la ufuta kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuagiza utumike mfumo wa zamani badala ya soko la bidhaa. Mfumo huo wa zamani unamruhusu mtu yeyote kwenda kununua maadam afuate taratibu zilizowekwa.
 
Bungu ni kibiti kiongozi sio Rufiji... Nilishituka nikazani upo Rufiji tupige kazi... Karibu Nyamwage Muhoro Miwaga...
Naam kuweni makini, dalili zinaonesha kwa mara nyingine tena mkulima wa ufuta atalia kilio cha mbwa koko. Tatizo ni Magufuli na serekali yake!. serekali ina migogoro ya kodi na wanunuzi wakubwa. Ina athiri vipi mkulima nitaeleza baadaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…