Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Mwanangu anatarajia kumaliza elimu ya msingi mwakani. Anasoma kwenye moja ya shule za umma (serikali) hapa Dar. Nisingependa aende kusoma shule hizi za kata ambazo nyingi mazingira yake ya elimu bado ni duni. Nilishindwa kumpeleka English medium Primary school , kwa sababu ya kutokuwa vizuri kiuchumi. Kwasasa nataka nijikakakamue mwanangu asome shule ya kueleweka. Nimeamua kuanza maandalizi mapema ili mwakani nisihangaike sana. Natafuta shule ambayo ada yake kwa mwaka haizidi sh.milioni 2. Tafadhali anayefahamu shule yoyote anijulishe.