Natafuta shamba - liwe kati ya Mlandizi na Dar

bhikola

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,131
Reaction score
1,663
Habari wadau,
Kama title inavyojieleza
Natafuta shamba, kuanzia ekari 4, liwe maeneo ya katikati hapo kuanzia Mlandizi kuja Dar.
Kuwe na maji au chanzo cha maji walau kwa umbali usiozidi kilomita 1.
Asanteni
 
Kwa upande wa dar sidhani kama unaweza kupata kwa kuwa sasa hata yale maeneo ya nje ya jiji wanauza viwanja na si mashamba ila kama pwani inawezekana kabisa ila kuanzia laki saba kwa eka
 
Mi nakaa Kibaha, nipe details zaidi. Umbali toka Morogoro road, bajeti, heka ngapi. Maeneo siyo shida. Au nicheki kwa 0713-039875
 
Kuna eneo, linafaa kwa ujenzi wa shule
Kigamboni, Chekeni Mwasonga, Linauzwa
Umbali =29km tokea ferry
Ukubwa = Takriban eka 10
Umeme = Nguzo 6 unafikia
Maendelezo= Kuna banda la vyumba 2 na frem ya duka
Kuna kisima cha maji matamu yanapatikana
Banda lishafanyiwa wiring
 
Kwa upande wa dar sidhani kama unaweza kupata kwa kuwa sasa hata yale maeneo ya nje ya jiji wanauza viwanja na si mashamba ila kama pwani inawezekana kabisa ila kuanzia laki saba kwa eka
Asante sana boss,
hata mimi lengo langu hasa ni mkoa wa Pwani, lakini zaidi upande wa kuelekea Moro, maana unaweza kuambiwa kisarawe au Mkuranga (MKIRU) huko ikawa balaa.
Mambo matatu kwangu ni muhimu kwa eneo husika: maji, kufikika, na usalama
 
Daaah
Mkuu hili eneo linafaa kwa kilimo/ufugaji kweli, maana inaonekana kama ni makazi ya watu zaidi.
Pia, nahitaji ekari kidogo tu siyo zote 10
Bei elekezi ni kiasi gani?
 
Mi nakaa Kibaha, nipe details zaidi. Umbali toka Morogoro road, bajeti, heka ngapi. Maeneo siyo shida. Au nicheki kwa 0713-039875

Mkuu asante sana kwa update hii
Kibaha ipi boss wangu?
Umbali kutoka Moro road isizidi 10km
Maji yawe yanapatikana karibu (unaweza kulima kwa kumwagilia)
Usalama uwe wa uhakika
Kuanzia ekari 4
Bajeti inategemea eneo husika, lakini reasonable farm price. (serching and connecting allowance included)
 
Habari wadau,
Kama title inavyojieleza
Natafuta shamba, kuanzia ekari 4, liwe maeneo ya katikati hapo kuanzia Mlandizi kuja Dar.
Kuwe na maji au chanzo cha maji walau kwa umbali usiozidi kilomita 1.
Asanteni

Shamba utapata Mlandizi karibu na eneo la viwanda ni wewe tu ujipange ili uonyeshwe site na baada ya hapo mapatano yataendelea...
 
Shamba utapata Mlandizi karibu na eneo la viwanda ni wewe tu ujipange ili uonyeshwe site na baada ya hapo mapatano yataendelea...

Sawa mkuu
Unaweza weka bei elekezi (walau price range) hata kama nakuja nikjue natagemea wapi mpaka wapi?
Muhimu kwangu ni kupata walau ekari 4 zilizo pamoja
 
Sawa mkuu
Unaweza weka bei elekezi (walau price range) hata kama nakuja nikjue natagemea wapi mpaka wapi?
Muhimu kwangu ni kupata walau ekari 4 zilizo pamoja

Mkuu bei elekezi haina nguvu sana pale mnapouziana eneo ambalo halijapimwa ingawa kwa sasa inacheza kati ya Tsh 6000 - 10,000 per Sq metre na inategemea zaidi na kiwanja kimekaa mahali gani, unayemuuzia ana ukwasi kiasi gani na muuzaji naye pia vyuma vyake vimekaza kiasi gani
 
Daah, miye mkulima ndugu yangu
kwa hiyo 6,000sqm maana yake karibu 3m kwa ekari. Mbali sana kwangu mkuu
miye nahutaji yale mashamba ya max 600k kwa ekari
 
Daah, miye mkulima ndugu yangu
kwa hiyo 6,000sqm maana yake karibu 3m kwa ekari. Mbali sana kwangu mkuu
miye nahutaji yale mashamba ya max 600k kwa ekari

Nimekupa estimate kama ulivyoomba lakini pia nimesema bei mara nyingi hutegemea vitu kadhaa kwa mfano je kiwanja kimekaa site ipi? huduma za jamii na miundo mbinu ikoje? je muuzaji ana njaa au shida ya pesa kiasi gani? na mwisho inategemea na hali ya mnunuzi ambapo ni wazi kuwa mwekezaji Mhindi hawezi uziwa bei sawa na wewe mkulima mzawa

NB: Matapeli wa Ardhi wametapakaa hasa huko Mlandizi/Pwani wakishirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, hili jambo shahidi mzuri ni Waziri wa Ardhi ambaye aliponea chupuchupu kuuingizwa mkenge na vishoka wazoefu
 
Nina shamba km chache kutoka Mlandizi kuelekea Bagamoyo, lenye mazao miembe ya kisasa na minazi imeanza kuzaa miaka 3 sasa...heka sh. 3.5M na Banda la vyumba 2 la tofari juu bati buree.... Pia kuna heka 4 @2M halina mazao.
Note: lenye mazao kuna kisima kirefu cha karavati. HAKUNA DALALI.
 
interested in this , embu namba zako za simu tuongee vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…