kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,899
Wakuu Salama,
Natanguliza shukrani kwa mawazo mazuri ambayo mnaweza nishauri.
Binafsi sina ujuzi wa mambo haya ila nimekuwa nikisia deals nyingi za namna hii zikiwa zimefanikiwa.
Mimi namiliki kiwanja chenye hati na ndipo nyumba yangu ya familia ipo. Ni eneo zuri lililo karibu kabisa na highway ya Mandela Road, sehemu ya Ubungo. Eneo hili linakuwa kwa kasi sana.
Nimewahi sikia wamiliki wengi kama mimi, wakipata deals na wawekezaji wakubwa ambapo huingia makubaliano ya Ujenzi wa majengo ya ghorofa na wao kujengewa nyumba ndogo za familia pembezoni mwa mji wa Dar es salaam.
Binafsi naomba mnielekeze naweza vipi kukutana na aina hii ya uwekezaji ambapo sipo tayari kuuza eneo bali nataka kuingia ubia na aina hii ya wawekezaji wa majengo marefu, tukubaliane shares na Ujenzi wa nyumba yangu ndogo ya familia nje ya mji, then nitakuwa tayari kwa deal la aina hii.
Najua hapa JF kuna wataalamu wengi wa mambo haya ya real estate [emoji537], naomba ushauri na mawazo yenu nitimize lengo hili.
Vijana wadogo wa shule ambao mada hii ipo juu kiupeo kwenu naomba, msilete comments zisizostahili.
Ahsanteni.