Natafuta shareholders kwenye biashara ya Wakala wa usafirishaji

Enny

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
962
Reaction score
130
Habari wana JF.

nilikuwa na wazo la kutafuta watu wa kuungana nao katika kufungua ofisi ya uwakala wa usafirishaji hapa Dar es salaam , Tunduma na Kyela.

Mimi nina lori moja scania la kusafirisha mizigo ya madukani tani 15. kwa sasa linafanya biashara ya kusafirisha mizigo toka Dar kwenda Tunduma.

nia yangu ni kupata watu wenye mtaji kidogo wa kukodisha ofisi na sehemu ya kuhifadhi mizigo ya watu kwa Dar na ikibidi kukodisha magari mengine kwaajili ya kusafirisha mizigo.

kama kuna mtu yupo tayari tafadhari ni PM tufanye kazi.

Asante
 
Vipi wana JF hamna watu walio interested jamani?
 
tuko interested lakini bado tunatafakari the way forward.

Hii ni business lazima ufanye evaluation kabla ya ku venture.
 
mimi nina truck(semi-trailer) moja linaloweza kubeba mpaka tani 30 pia container ya 20 na 40. Nipo interested kujua zaidi kuhusu idea yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…