Natafuta soko la Limao nipo Morogoro

Shuku_

Senior Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
174
Reaction score
216
Poleni na majukumu wana JF, Natafuta soko la Limao

Lengo la kuanzisha uzi huu ni kushirikiana na mdau yeyote.

Kama wewe huko ulipo bei inalipa basi tushirikiane na nna uwezo kukusanya tenga moja kwa siku lenye malimao 1,000 hadi 1,500.

Manunuzi :- Kuhusu bei ya kununulia kwa huku ni 50 tsh limao dogo na kubwa ni 100 tsh.

Natanguliza shukrani kwa wale wadau ambao hawatakuwa wachoyo wa kununyima ushirikiano ktk mchongo huu.

 

Attachments

  • FB_IMG_15673136868123964.jpg
    70 KB · Views: 46
Mimi niko dar cha msingi weka mawasiliano yako hapa watu wakutafute
 
Kuna swali hua najiuliza,hivi haya malimao ninayo yaona kila siku sokoni maana yake kuna watu hua wamelima milimao au?Na kama yapo ni mikoa gani wanalima?

Maana sijawahi kuona mashamba ya malimao kama ambavyo nimeona ya machungwa/machenza.

All the best mtoa mada.
 
by the way bei ya chungwa Tanga shambani ni 20/= best kabisa lile bora ni 50/=
Mkuu inatakiwa ujue kitu kimoja kinaitwa “UMUHIMU”.

Kila kmoja kina umuhimu wake kwaiyo huwezi kumsema chinga anayetaka kukuuzia kofia kwa elfu 15 “eti sasa chinga mbona unauza kofia bei ghali ivo sa si bora nkanunue raba pea 3 za elfu 5,5 kwa bei hiyo”.
 
Nilichogundua hapa kwenye huu Uzi wengi hamjui kuhusu malimao . Malimao kibiashara yako hivi
Kuna msimu Malimao ni mengi sana kama kuanzia mwezi wa Pili mpaka wa Tisa hivi
Na kuanzia mwezi wa kumi Malimao hayapatikani sana mpaka mwezi wa kwanza.
Kwasababu kipindi hicho(10-1) mwezi Malimao huwa yanapatikana mpaka Uganda huko kuja moshi na dar.
Sasa na hiki ndicho kipindi ndo maana unaona yanauzwa bei ghali sana.

Jaribu kujua nyakati
 
Huko mashambani uuze limao 1 sh 50 hadi 100 umekosa soko kabisa na mjini watauzaje maana ndo bei za mjini malimao 4 makubwa 500 kutoa huko bado usafiri...
Soma oni zlizopta kabla ya changia oni lako.
 
Morogoro upo sehemu gani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…