Natafuta tani 50 za Mianzi (Bamboo)

mkuu niunganishe na hao jamaa nichukue chngamoto mana hata mm nipo kwenye huo mchakato
 
Mkuu Iringa wilaya zipi ambazo ninaweza kupata kwa wingi? Maana Iringa ni kubwa
njoo mtwivila, kalenga na isimani..kwanza picha linaanza utapiga ulanzi wee hadi uombe pooo, halfu tunaingia kukata mianzi! nna shamba kubwa sana ntakuuzia mwani mmoja tsh 250.
 
Kuna mianzi ya ulanzi na mianzi ya kawaida.! Mianzi ya ulanzi ni milaini sana na inakuwa mifupi sana. mianzi ya kawaida ni minene na mirefu japo inategemea na sehemu ilipooteshwa.!

Upatikanaji wake ni mgumu sababu ile haipandwi mara kwa mara, ukiona msitu wa mianzi ujue hapo ni mahame imepandwa enzi za (sogesa.), Kwa zamani ilikuwa inatumika kwa ujenzi na uezekaji wa nyumba, ususi wa vikapu na nyungo.....Ila sasa hivi sababu watu wanajenga nyumba za matofali na kuezekea mabati mianzi inazidi kupotea taratibu sababu umuhimu wake unapungua siku hadi siku.

Naongea kulingana na uzoefu wangu Makete.!
 
Changamkieni fursa, ila msisahau kupanda pale mnapokata
 
mkuu jajcom .... swali la msingi kabla ya kupata source ya mianzi (Bamboo) .... Je unataka mianzi kwa matumizi gani? ..... Kwasababu kuna aina (spicie) zaidi ya 100 za bamboo na kila spicie ina characteristics, properties and behaviours tofauti katika matumizi
 
Ipogoro, kilolo, dabaga, ifunda, kidamali, mufindi, hizo ni sehemu za kupata mianzi makini kwa mkoa wa iringa, kule vijijini. Tani zote unavuna hapo
 
Minazi ipo yakutosha moshi wala haipo chini ya usimamizi wa maliasili karib
 
Mkuu kama unampango wa kuanzisha kiwanda cha Toothpaste nakupa bigup. Tutolee hii aibu ya kutumia TP toka china
 
Kule kagera ipo. Ukikosa uko kachukue kagera hata tani 200 utapata
 
OK

Ngoja niwasiliane na MAAFISA MISITU wenzangu nijue ni wapi utapata mzigo wa kutosha. Ila itakuwa ni huo ukanda wa coastal regions
Mkuu, naomba utaratibu wa kupata kibali cha haraka ili kuvuna na kusafirisha mbao
 
Mkuu njoo Nachingwea lindi Tanzania utaipata
 
Mkuu nashukuru sana, Naweza kupata mawasiliano ya mkazi wa hayo maeneo?
Iringa na Njombe kuna mianzi midogo (Miembamba) ya Ulanzi hakuna mianzi (minene), Ulanzi hutoka kwenye mianzi membamba(fito), mianzi minene ipo Morogoro Milima ya uluguru wanatengenezea matenga ya kubebea ndizi, au mifumo ya kitamaduni ya kuvutia maji. Utaipata mingi lakini kwa sasa ni gharama maana kila mtu analinda mashina yake. Nenda Matombo ndani, kanisa katoliki, utawakuta Waluguru wanasukia ndizi, wape ramani, ndani ya wiki utapata TANI 30.
 
Jamani mbona wenye viwanja mko kimya jamani watu wa kibha picha ya ndege njooni mnpe eneo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…