Natafuta trekta

Kuna sehemu pale moroco barabara ya kwenda nyumbani kwa Kikwete unaweza kupata tractor imara na durable za John Deere pamoja na implements.
 
Unatak mpya au used?

Unataka uliyotumika hapa Tanzania au Nje?
 
Mkuu nimekupata!!!

Tafadhali, baada ya kufuatilia kwa makini hoja hii, kwanza ningekushauri utoe unyambulisho wako kama ifuatavyo:-
  • Angalao toa aina mbili za trecta unazohitaji kutokana na mazingira / maeneo / mikoa unayoenda ku-invest, hii itasaidia kuja utakutana na udongo wa aina gani? Spares nazo zina - matter sana hususani utakapo kuwa upo busy, spares sometimes huwa zinasumbua sana.
  • Kutokana na uzoefu wangu, baadhi ya Models ambazo piga ua, utapata spares aina yoyote kwa ukaribu zaidi hata kama upo Kiteto, Mbarali au Kilindi, hapo hujagusia Moro na Central Zone, mwanangu kwanza ni Massey Ferguson, Ford, John deer na International. Zote hizi unaweza kupata Used tractor nzuri kutoka U.K / Holland. Spares / Accessories zake zipo za kumwaga.
  • Kuwa specific na HP na hii itazingatia in long run unataka kufanyia nini na hiyo tractor, pia inategem,ea hiyo tractor ifanya shughuli zipo wakati haipo shambani kwani tractor unaweza fanya mambo yote hata wakati wa ujenzi.
  • Ningekushauri pia angalia uwezekana wa kuagiza moja kwa moja kutoka nje, U.K sio mbali, within siku 28 unakuwa na Tractor yako, hizi za hapo mjini elewa kabisa kuwa lazima kuna hela fulani ya mtu wa kati au hata kama ni mtu pekee kaa-giza kutoka nj lazima utamwekea faida yake hapo, matractor siku hizi hata ukitembelea website ya TRA, kuingiza ni bure. Ka kuanzia ukisubiri yako unaweza kukodisha yako na kuanz kazi zako kabila ya mvua za huko Kilindi / Moro hazijaanza.
  • Kama ungependela matrector kutoka u.k, tembelea www.farmerstrader.com au www.fwi.com then ukisha chagua tractor yako tafuta mtu aliyopo U.K akakuangalizie hilo tractor na kukusaidia kulisafirisha, of course hapo utampa / utampooza na kitu kidogo kwani mafuta u.k ni ghali kidogo na si unjua tena mpaka mtu aache shift yake kwenda kukufuatilia tractor yako North, i.e Yorkshire, kuna ka umbali kaka. Ni - Pm nikuunganishe kama utapenda hii Idea, nina mtu yupo U.K.
  • Umesema unataka kununu hapo hapo Dar? Hjasema Budget line yako ni kiasi gani? Upo tayari kutoa kiasi gani kwa used tractor i.e Mf 100 - 600 Series? Nikiwa na maana kuanzia MF (Massey Ferguson) 165, 168 175, 240, 290. 565, 590 n.k hizi ni baadhi tu.
  • Mkuu mashamba umepata wapi? Tupeane Desa / Simbi mkuu wangu??
  • Matrector ya China, india, Paksatani sio imara sana kama ya U.K / Holland
Tupo wote, chacharika kabla ya mvua hazijawa nyingi
 
Mkuu naamini hili nilishajibu hapo juu kuhusu geographic location.... in fact i could even go for 2 if the price is right


Mkuu hapo tuko pamoja ila i would prefer Massey, Kubota or John Deer... kuhus specs, mimi sio mtaalam na ndio maana kwenye post #1 nimetoa project but now i want a product... i am also worried naweza nikachelewa so ningependa kuchukulia Dar

I am hopeful kwamba by next monday ntakua na moja......

Kuhusu bajeti na baadhi ya dditional question mkuu, ndicho kilichonileta hapa, na nina experience ya bongo, ukisema una milioni kumi basi hata cha laki tano watakupa kwa milioni kumi!!!! in other words i would like to keep my cards about price on my chest

Nimekusanya maoni na kuamua ijumaa ntafanya serious trip na ikibidi kuchukua kabisa mzigo

muda umenitupa mkono
 

Kama unaweza kunipatia contacts zake ntashukuru maana mi ninalo tractor ila ningependa kupata jembe(mpini) toka malawi.
 
Kuna jamaa anaenda Malawi anakuja na Massey nzuri na bei yake huwa around 9-12 Million.yeye ni fundi huwa anaenda kununua spares na off-farm tractors.anapatikana mpakani mwa malawi na Tz.
Miezi 4 iliyopita alikuwa na Tractor zuri.hali yangu haikuruhusu sikuweza kulichukua.
Jamaa anaitwa Chawinga ni maarufu sana pale border na anaweza kudeliver to your location

Naomba na mimi unisaidie na contact zake tafadhali nahitaji kununua tractor...Unaweza wasiliana nami kupitia shirleysprouse@ymail.com
 
Nunua MF na Ford kakini pia model gani. Usifanye haraka wala usifikirie sana kununua jipya. Matrekta ya zamani ni imara kuliko ya sasa. Kama utapata ford 800 au 810 hapo una trkta. MF 286/386 moja lao pia zuri
Usinunue kabisa matrekta ya sumajkt utajuta na utanikumbuka Farmtrac new Holland ya India usichukue. Kama wapata new Holland ya ulaya chukua. john deer itakuhangaisha
KUMBUKA: usinunue trekta za suma jkt
 
Mkuu za suma jkt Zina matatizo gani.
 
Trector mpya ya massay kutoka uk.. Contact 0752039770

Mkuu naona umekosea hiyo itakuwa ni used kutoka Uk Massey mpya zinatoka Pakistan mpya ya Uk? Hapana ni massey model gani hiyo kama ni mpya kwa Mtanzania wa kawaida ataiweza bei yake kweli
 


Massey Ferguson 265 4wd £7,750



Massey Ferguson 6150 4wd tractor £12,450



Ransome TS 90 4 Furrow Plough £525



Stamford/Perkins 100 KVA Generator £7,250

For everything else visit http://www.howardandsons.co.uk/




Hakuna longolongo hapo unataka kulima unayo hela yako just about anything is available better still delivered to your port, vema kama una ndugu na jamaa wakujaribisha tu just to get the second opinion yaliyobaki bidhaa ya bei unabishana mwenyewe provided lugha inapanda.
 
Hp ngapi?
Nahitaji huduma hiyo nipo mkuranga magoza.
Ardhi ni ngumu haijalimwa siku nyingi kama trekta lako lina uwezo wa kulima kuanzia kina cha nchi 4 nikupe kazi
 
Msaada wa namba zake tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…