Moseley
Senior Member
- Jul 10, 2010
- 187
- 98
Habari ndugu zangu!
Napenda kuweka wazi kuwa sina haja ya kuendelea kuitwa Mtanzania kama chama tawala cha sasa kitaendelea kushika hatam oct 31..
Kwa maana hiyo, sina haja ya kujivunia kuwa mie ni mtanzania, wakati mambo yanakwenda hovyo..
Sababu:
1. Chama tawala kinatumia ujinga wa watanzania kama mtaj wa kutawala milele..
2. Chama hicho hicho hakifanyi juhudi ya kuwapa elimu watu wake kwa maana wanatambua fika kuwa wananchi wakipata elimu hawatakubali kutawaliwa HOVYO na chama hicho..
3. Chama hicho hicho kinamiliki jeshi, mahakama na kimekuwa kikiendelea kuwa na wabunge wengi ambao wapo pale kwa matumbo yao....
4. Chama hicho hicho kinamiliki rasilmali nyingi kuliko vyama vingine, kiasi kwamba hakuna ushindani sawa wa kisiasa, kwa maana hiyo hakuna Demokrasia ya kweli... Kwa hili nachelea kutoa lawama kwa baba wa taifa ya kwamba kwa nini HAKUIPASUA CCM kabla hajaondoka
Tulitegemea kulikoa taifa kwa nguvu ya umma, Ila hatujaweza kuwaelimisha watu kiasi cha kutosha kutokana na rasilimali chache zilizopo kwa wanaharakati na nyingi kuegemea upande wa chama tawala ambacho hakitaki elimu ipatikane kwa wananchi.. Maana wananchi wakiwa na elimu, utawala huo utakufa...
Kutokana na maneno hayo natangaza rasmi kuanzia tarehe 31 oct, nisiitwe mtanzania kwa maana sina cha kujivunia..
Na kwa maana hiyo naomba watu wanaoweza kunisaidia kupata uraia wa Botswana, Ghana , US , Uswisi au Australia wanisaidie.. Hata kama huko nako kutakuwa na matatizo, naamini sio kama ya hapa kwetu nyumbani
Shukrani