Natafuta viatu vya kunyoosha miguu kwa ajili ya mtoto mwenye matege

Natafuta viatu vya kunyoosha miguu kwa ajili ya mtoto mwenye matege

Mkonowatembo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2016
Posts
1,107
Reaction score
1,012
Poleni na kazi na majukumu ya kutafuta riziki. Jamani mwanangu ana matege nimetumia dawa za vitamini D lakini bado sioni mabadiliko ana miaka miwili sasa.

Je, wapi nitapata viatu vya kunyoosha miguu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KCMC kuna kitengo cha kutengeneza hivyo viatu
 
Wazo la mwamba hapa ni zuri Sana Mimi wa kwangu ilinyooka vizuri gharama kwa upande wetu ilikuwa ni kuhudhuria tu clinic.
Mkuu jambo la muhimu ni mtoto afike hapo CCBRT aonwe na wataalamu ambao watampima na kugundua kuwa viatu vitatosha kumpatia matibabu au operation itamsaidia mtoto, kuwahi mapema ni muhimu sana katika matibabu haya la sivyo mtoto atakuwa kilema maisha yake yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jambo la muhimu ni mtoto afike hapo CCBRT aonwe na wataalamu ambao watampima na kugundua kuwa viatu vitatosha kumpatia matibabu au operation itamsaidia mtoto, kuwahi mapema ni muhimu sana katika matibabu haya la sivyo mtoto atakuwa kilema maisha yake yote.
Umemshauri vyema, maana mara nyingine huwa wanamshauri tu mzazi vyakula vya kumpatia mtoto mpaka anakuwa sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu fata ushauri wa wadau mtoto anyooke miguu
 
wangu alikuwa nayo kwnye mwaka mmoja hivi kufika miaka 2 yaliisha yenyewe
 
Heri yako mkuu. Mimi wiki iliyopita CCBRT wameninyoosha laki tatu na arobaini kwa viatu hivyo.
Ok nimeenda ccbrt mwezi wa tatu sasa wananipa vitamini D tu ila bado anaendelea na vodonge vya vitamini D vikiisha nitaenda kuwasililiza wataalamu nashukuru kwa ushauri wenu mbariiiwe wa JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom