Natafuta wabia wa kujenga kuendesha na kuhamisha (build operate transfer)

aligawee

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
507
Reaction score
105
Wadau Habari za jamvini.
Nina jengo langu maeneo ya kibaha picha ya ndege ambalo ni mahsusi kwa kupangisha. Nimejaaliwa kuongeza vyumba vitano ambavyo vimekamilika tayari kwa kila kitu isipokuwa Madirisha ya aluminium. Ninamtafuta mdau makini (genuine) ambaye atakuwa tayari kuingia mkataba nami wa kumalizia kazi iliyobaki na kisha kukusanya kodi na faida yake kwa muda tutakaokubaliana kisha aniachie mjengo wangu.
Akipatikana mdau wa kukubali kukarabati pia jengo la zamani itakuwa bora zaidi na asiwe na wasiwasi kwani utakuwa ni uwekezaji kama ulivyo uwekezaji mwingine wowote. Huenda uwekezaji huu ukawa na faida kubwa zaidi. Yeyote mwenye nia tuwasiliane 0621107223
 
Hiyo build operate transfer (BOT) itakuwa ngumu kwa hapo ulipofikia mara nyingi miradi hiyo huanzishwa wakati ujenzi haujanza na ni mkataba makini. Kwa hapo ulipofikia tafuta anaetaka kupangisha alipie kabla kisha utumie hiyo pesa kumalizia ujenzi. Nadhani umefika mbali kushindwa kumalizia, madalali wanaweza kukusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…